Mimi nimeteuliwa kuwa Mrithi Mkuu katika Familia yetu, kila ndugu yangu amepewa mali yake kwa mjibu wa wosia wa Marehemu ambao uliandikwa na Maremu baba yetu enzi za uhai wake kupitia kwa Wakili. Ila baada ya miaka 11 ndugu zangu wameibuka na kupeleka mashtaka mahakamani kwa lengo la kutaka wagawane mali zangu ambazo nimeziendeleza kwa miaka 11. Izingatiwe kila mtu (mimi na ndugu zangu) alikubaliana na mgawo uliotolewa kwa kusaini na nyaraka zipo. Je kisheria kuna uhalali wa mimi kunyang'anywa mali zangu hizo???
Naomba msaada wa kisheria juu ya hili.