Sheria ya ndoa: Haki na wajibu wa mume/mke katika ndoa

Sheria ya ndoa: Haki na wajibu wa mume/mke katika ndoa

mka

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2010
Posts
318
Reaction score
82

HAKI NA WAJIBU WA MUME NA MKE KATIKA NDOA KISHERIA SEHEMU YA 1

Maana ya ndoa
Ndoa maana yake ni muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao yote (Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971). Ili ndoa hiyo iwe halali hapa nchini inapaswa kufuata matwaka ya Sheria za Tanzania kama:

Muungano lazima uwe wa hiari, muungano uwe ni kati ya mwanamke na mwanaume, muungano huo uwe unakusudiwa kuwa wa kudumu, wafunga ndoa wawe wametimiza umri unaokubalika kisheria, wafunga ndoa wasiwe maharimu (wasiwe watu wenye mahusiano ya karibu ya damu au kindugu), kusiwe na kipingamizi na mfungishaji ndoa awe na mamlaka ya kufungisha ndoa.

Aina za ndoa
Kulingana na Sheria ya Ndoa kuna aina kuu mbili za ndoa; ndoa ya mke mmoja na ndoa ya zaidi ya mke mmoja. (Ifahamike kwa Sheria ya Tanzania mke anapaswa kuwa na mme mmoja tu).

(a)Ndoa ya mke mmoja

Huu ni muungano unaoruhusu mwanamme kuoa si zaidi ya mke mmoja. Mfano, ndoa ya Kikristo.

(b) Ndoa ya zaidi ya mke mmoja
Huu ni muungano unaoruhusu mwanamume kuoa mke zaidi ya mmoja. Mfano, ndoa za Kiislamu na ndoa za kimila.

Sheria ya Ndoa inatambua aina tatu za ufungaji ndoa yaani kiserikali, kidini na kimila. Pamoja na aina za ndoa zilizotajwa hapo juu sheria ya ndoa inatambua dhana ya kuchukulia ndoa hii ni kwamba iwapo itathibitishwa kwamba mwanamume na mwanamke wameishi pamoja kwa muda wa miaka miwili au zaidi na kupata heshima ya mume na mke basi itakuwepo dhana inayokanushika kwamba watu hao walioana ipasavyo. Madhumuni ya dhana hii ni kumwezesha mwanamke na watoto kupata masurufu pale ambapo ndoa inavunjwa.

HAKI NA WAJIBU WA MUME AU MKE KATIKA NDOA
Baada ya kufunga ndoa na ikaonekana haina kasoro yoyote, mke na mume aana haki mbalimbali kisheria anazostahili kuzipata kisheria. Haki hizi ni kama;

Matunzo
Mke au wake wana haki ya kutunzwa na mume wao kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama chakula, malazi, mavazi, matibabu, n.k kulingana na uwezo alionao mume. Hivyo katika ndoa mume anao wajibu wa kumkimu mkewe kwa kumpatia malazi, Nguo na chakula. Mke mwenye kipato vile vile anao wajibu wa kumkimu mumewe ikiwa tu mume huyo:
· Hajimudu kabisa.
· Hawezi kupata chumo la Maisha yake kwa sababu ya athari ya akili au afya mbaya
(hii ni kwa mujibu wa Sheria ya ndoaSura ya 29 ya sheria kifungu 63).

Hivyo basi kisheria mume ndio mwenye wajibu wa kwanza wa kumtunza mkewe. Mke anaweza kumtunza/kumkimu mume ikiwa mume hajimudu i.e hawezi kufanya kazi au shughuli kwa sababu mbalimbali kutokana na athari ya akili au akiwa na afya mbaya. Ikumbukwe mke anaweza kudai kwenye vyombo vya kisheria ikiwemo mahakama kama mume hatampa matunzo.

kutunza watoto
Mume na mke wana wajibu wa kumtunza na kumhudumia mtoto wao na kumpatia mahitaji muhimu kama chakula, nguo, malazi, elimu na mahitaji muhimu. Ni kosa kisheria kutokumuhudumia mtoto wakati ukiwa na uwezo wa kumhudumia. Makosa hayo ni:

Kutelekeza Watoto
Kwamba mtu yeyote ambaye, ni mzazi au mlezi au mtu mwingine mwenye uangalizi au utunzaji halali wa mtoto yeyote mwenye umri usiozidi miaka kumi na nane, hali ana uwezo, wa kumuhudumia mtoto, kwa kuamua au kinyume cha sheria, au bila ya sababu za msingi atakataa kumhudumia, na akamtelekeza mtoto bila msaada, atakuwa ametenda kosa. Kifungu cha 166 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya sheria za Tanzania pamoja na kifungu cha 188 cha Sheria ya Mtoto ya 2009.

Kosa la Kupuuza kumpa chakula mtoto n.k
Mtu yeyote ambaye, ni mzazi au mlezi au mtu mwingine mwenye uangalizi au utunzaji halali wa mtoto yeyote mwenye umri usiozidi miaka kumi na nne na asiyejiweza, akakataa au kupuuza (hali ya kuwa anaweza kufanya) kumpa chakula cha kutosha, nguo, malazi na mahitaji mengine ya lazima kwa maisha ya mtoto kiasi cha kumdhuru kiafya mtoto huyo, atakuwa ametenda kosa. Kifungu cha 167 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya sheria za Tanzania pamoja na kifungu cha 189 cha Sheria ya Mtoto ya 2009.

Umiliki wa pamoja wa mali na mahusiano baina ya wanandoa
Mali ya mke au mume iliyopatikana kutokana na jasho lao wote wawili ni mali yao kwa pamoja hata kama juhudi zao au jasho lao katika kupata mali hizi si sawasawa. Lakini pamoja na hayo kuna dhana inayokanushika kuwa kama mali hii imeandikishwa kwa jina la mmoja wao basi ni mali yake. Ni wajibu wa yule anayedai kuthibitisha kuwa pamoja na kwamba mali pamoja na kwamba mali imeandikishwa kwa jina la mwenzake, ni mali yao kwa pamoja. Mwanandoa huyo anaweza kuthibitisha kwa kuonyesha kwamba amechangia jasho lake mfano kwa kuendeleza, kuzalisha au kuboresha mali hiyo. yule mwanandoa aliyechangia atakuwa amepata haki ya kumiliki ile mali kwa hisa ya pamoja (occupancy in common) na yule mwenye haki ya kumiliki ardhi.

Mke au mume ana haki ya kumiliki mali aliyoipata kabla ya ndoa kama aliipata kwa fedha yake mwenyewe ingawa mwenza (mume/mke) ana haki kama ilivyoelezwa hapo juu akonyesha kuwa amekuwa akichangia kuiendeleza au kuitunza. Pia Mke ana haki ya kuingia mikataba, kushitaki na kushitakiwa kwa jina lake mwenyewe. Makubaliano yaweza kufanywa na wanandoa hiyo jinsi ya kumiliki mali iliyopatikana kabla ya ndoa yao na jinsi gani waimiliki.

Kwa mali iliyopatikana wakati wa ndoa, mali hiyo ni mali ya wanandoa wote, kwa sababu imepatikana kwa mchango wa nguvu za pamoja. Hii haijalishi kuwa mmoja wa wanandoa (mke kwa mfano) hachangii pesa tasilimu au anakaa nyumbani na kufanya shughuli za nyumbani tu. Kufanya shughuli za nyumbani ni mchango mkubwa na ameokoa fedha nyingi.

Sheria ya Ardhi Sura ya 113 inaeleza kuwa pale mwanandoa anapopata ardhi kwa matumizi ya wanandoa wote au mwanandoa mwenzake, kutakuwepo na dhana kuwa hawa wanandoa wanamiliki ardhi kwa pamoja kwa hisa zinazogawanyika (occupiers in common). Kama dhana hii haitabatilishwa basi Msajili wa Hati atawaandikisha hawa wanandoa kama wamiliki wa pamoja wa hisa/maslahi zinazogawanyika (Occupiers in common).

Haki ya kukopa kwa dhamana ya mume;
Wajibu wa kutunza mke na watoto ni wajibu wa mume au baba kwanza. Kwa msingi huo, endapo baba amesafiri, haitunzi familia, au ametoroka na baadaye matatizo yakajitokeza yanayohitaji fedha, basi mke ana haki ya kukopa fedha kwa jina la mume au kuweka rehani mali ya mmewe. Ifahamike kwamba mke anaruhusiwa kukopa kwa ajili ya mahitaji muhimu tu ya familia na kwa kuangalia pato la mumewe.

Jambo la kuzingatia kwa makini hapa ni kuwa ili haki yakutumia mali ya mume iweze kuwapo ni lazima mahitaji yanayonunuliwa yawe ni yale ambayo kama mume mwenyewe angekuwepo angekuwa na uwezo wa kuyanunua kulingana na pato lake

Haki ya kuishi katika nyumba ya Ndoa;
Nyumba ya ndoa ni nyumba ambayo mke na mume wanaishi wakati wa ndoa. Hata kama wanandoa wana nyumba nyingi, basi wanayoishi au kutumia kama makazi ndiyo nyumba ya wanandoa. Nyumba hii haiwezi kuuzwa, kuweka rehani au kuchukuliwa na mtu mwingine kama zawadi bila ya makubaliano ya wanandoa wote. (bila ridhaa ya wanandoa). Mwanandoa ana haki ya kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka amri ya mahakama ya kuvunja ndoa, au kutengana itakapotolewa.

Asanteni karibuni, Itaendelea…

NB: Karibuni wanaJF kwa maoni na maswali.
 
elimu inangia ila haya mambo ya ndoa yanahitaji kuwa handled makini na kwa busara sana ili kuepuka kuhatarisha ndoa kwani ndoa ni sakrament ya Mungu na ni taasisi kubwa kuliko taasisi nyingine kwani ndo chimbuko la uhai na uimara wa taifa pia
 
Inabidi uweke na sharia zitakazosimamiwa na Kadhi, kwani wapo watakaotaka wakahukumiane huko

Mkuu hilo tusubiri kama mahakama ya kadhi itaanzishwa huku bara tutajua.
 
elimu inangia ila haya mambo ya ndoa yanahitaji kuwa handled makini na kwa busara sana ili kuepuka kuhatarisha ndoa kwani ndoa ni sakrament ya Mungu na ni taasisi kubwa kuliko taasisi nyingine kwani ndo chimbuko la uhai na uimara wa taifa pia

Mkuu Sheria ya Ndoa, 1971 imetambua ndoa zinazofungwa kulingana na imani za wafungaji. Mfano ndoa ya kikristo yapaswa kua kuwa ya mke mmoja. Hapa tumekumbushana wajibu Wa mwanandoa na ukisoma wajibu utajua kuwa mwanandoa akiufuata atakuwa anailinda sakramenti hiyo (Kwa wakristo).
 
Mkuu mka, kanisani huwa tunaambia kuwa tumekuwa mwili/kitu kimoja. Swali ambalo sijapata majibu, kwa nini sasa kila mmoja anapewa hati yake ya ndoa? Kuna nini hapo?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mka, kanisani huwa tunaambia kuwa tumekuwa mwili/kitu kimoja. Swali ambalo sijapata majibu, kwa nini sasa kila mmoja anapewa hati yake ya ndoa? Kuna nini hapo?

Mkuu Polisi cheti cha ndoa ni ushahidi kuwa mmeoana. Hivyo Kila mwanandoa anapaswa kuwa na nakala yake. Pia cheti cha ndoa kinatolewa na Serikali siyo kanisa. Mfungisha ndoa awe Mchungaji au padri (Kwa wakristo) anapewa leseni na serikali ikionyesha ana mamlaka ya kufungisha ndoa. Na akitoa cheti cha ndoa anakitoa kwa niaba ya Serikali.
 
Last edited by a moderator:
elimu safi sana hii,kumbe hizi za siku hizi za mikataba na zile za 071.. hazikubaliki? thanx sana
 
elimu safi sana hii,kumbe hizi za siku hizi za mikataba na zile za 071.. hazikubaliki? thanx sana

Mkuu kulingana na Sheria za Tanzania ndoa inapaswa kuwa Kwa madhumuni ya kudumu sio Kwa muda. Pia ni kati ya mwanamke na mwanaume. Pia mwanamme na mwanamke wanapaswa kuwa walizaliwa na jinsia zao hizo sio kwa kubadili jinsia.
 
Haki ya kuishi katika nyumba ya Ndoa;
Nyumba ya ndoa ni nyumba ambayo mke na mume wanaishi wakati wa ndoa. Hata kama wanandoa wana nyumba nyingi, basi wanayoishi au kutumia kama makazi ndiyo nyumba ya wanandoa. Nyumba hii haiwezi kuuzwa, kuweka rehani au kuchukuliwa na mtu mwingine kama zawadi bila ya makubaliano ya wanandoa wote. (bila ridhaa ya wanandoa). Mwanandoa ana haki ya kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka amri ya mahakama ya kuvunja ndoa, au kutengana itakapotolewa.

Asanteni karibuni, Itaendelea…

NB: Karibuni wanaJF kwa maoni na maswali.

Hapo mbona sheria inakinzana, kwa mfano mwanandoa mmoja alikuwa na nyumba kabla ya kuoa au kuolewa ambayo hapo awali umesema hiyo ni mali yake though mwanandoa anatakiwa athibitishe namna alivyochangia nguvu yake katika kuitunza, assume hajachangia chochote alafu hiyo nyumba ndio wanandoa wameamua kuishi miaka nenda itachukuliwaje ni nyumba ya ndoa wakati imejengwa na mmojawapo kabla ya ndoa
 
Nyumba ambayo ina usawa kati ya mke na mume ni ile ambayo walijenga pamoja, endapo watataka kukopea mkopo bas consent ya wote wawili itahitajika.
 
Hivi kama sheria inatambua ndoa ya Watu walioishi pamoja miaka miwili....sasa je, nao wanayo haki ya kuomba talaka mahakamani kama Wanandoa wengine?

Sasa kuna haja gani ya kutambua ndoa za aina hiyo ikiwa ndoa za kawaida zimewekewa miongozo na sheria ambazo zikikiukwa hamfungishwi ndoa..kwa mfano kukiwepo pingamizi ndoa haifungishwi..Mfungishaji asipokidhi vigezo hawezi kufungisha ndoa n.k.

Mambo yanayobatilisha ndoa zinazofuata taratibu sahihi yanafanyaje kazi kwa ndoa ya waliojiamulia tu wenyewe kuishi pamoja?...nahisi kuna mkorogano hapa.
 
Kuna haki za watu walioishi pamoja zaidi ya miezi sita na ndio sababu mojawapo ya kuhesabiwa kama wanandoa.
 
Back
Top Bottom