Sheria ya ndoa: Haki na wajibu wa mume/mke katika ndoa

Nadhani Sheria iongezewe vifungu kutokana na kuongezeka 'wasaidizi ndoa' au michepuko ili na yemyewe ipate haki
 

Mka, Elimu hii ni nzuri sana sana isipokuwa naomba kuuliza mambo yafuatayo

1. Je ndoa haizungumzii kuhusu hali ya wanaotaka kufunga ndoa kabla ya ya kufunga ndoa?
a)mwanamke kutokuwa bikra au kuwa ameshazaa na mtu mwingine kabla ya ndoa?
b) sijui ni semeje labda na mwanaume kutokuwa bikra au alishawahi kuwa na motto kabla ya ndoa?
Wanajamvi tukubaliane kuwa hali hizi huleta misukosuko sana katika ndoa kwani ni kibinadamu kuwa wazazi wenza wa watoto waliozaliwa kabla ya ndoa hizo ama hutamani kuwaona na kuwatunza watoto wao au kujikumbushia Enzi zao kabla hawajakutana na waume au wake wa ndoa.

2. Uwezo wa kujaza mimba au kubeba mimba.
Je hili katika ndoa likoje kisheria, je ndoa ni makubaliano tuu ya kusishi pamoja kwa muda wa maisha ya wanandoa? Je kama mwanandoa hawawezi kuzaa kuna ndoa hapo? Sheria inampa mume jukumu la kutunza watoto, je unatunza watoto wepi kama mmoja hawezi kuzaa

3. Kuendelea kuzaa na mzazi wa kwanza kama mwanandoa mwenza hana uwezo wa kuzaa
a) Je kuna kosa kisheria
b) Ikitokea kuwa mwanandoa ama hana uwezo wa kubeba mimba au kubebesha mimba, je mzazi mwenza wa kwanza akiendelea kuzaa na mwanandoa kuna kosa kisheria?
4. Mfano, mlikuwa marafiki wawili, Mwanamke akapata Mimba, kwa sababu moja au nyingine hamkuweza kuoana, kila mtu akaenda zake akasonga na maisha. baada ya miaka 3 mwanamke akaolewa na mwanaume akaoa. Imetokea ama mke au mume huko alikoolewa au ulikooa kuna matatizo hawapati watoto. mwanamke akamtafuta mwanaume na kumsihi kuwa huko aliko mume hana uwezo wa kumtia mimba hivyo motto wao amekuwa mpweke anahitaji mdogo wake. mwanaume akatekeleza ombi la mwanamke motto akapatikana hivyo mwanamke ana watoto wawili na wote kawaandikisha ubini wa mwanamme asiyezaa. aliyemzalisha hana motto katika ndoa yake na anawataka watoto wake. wa kwanza si shida kwani hajazaliwa ndani ya ndoa. Je wa pili atafanyaje? maana yule mwanaume asiyezaa anaamini kuwa ni mwanae?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…