Upo sahihi sana
Sheria ya ndoa nadhani ni mojawapo kati ya sheria zinazohitaji kuwa reviewed, ipo biased sana.
Ukiwa na mali yoyote kabla ya ndoa na ikawa imeandikishwa kwa jina lako, itahesabiwa ni yako, ukioa, kama mkeo hajawahi ijua na hajawahi kujishirikisha kwa namna yoyote ktk mali hiyo itahesabiwa ni yako mkitengana, lakini tu, akijishirikisha vyovyote vile na mali hiyo, itahesabiwa amehusika kuiendeleza na mtagawana 50/50.
Mali zote mlizopata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikwa jina la mume, mtagawana 50/50, lakini tu, ikitokea mmezipata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikishwa kwa jina la mke, itahesabiwa kuwa ulimpa zawadi, na ni "transfer of ownership" na kwakweli hizo hupati hata senti tano.
ANGALIZO; Kuweni makini na mali mnazowaandika wake zenu!!!