Sheria ya ndoa lazima ibadilike

kahtaan

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2009
Posts
18,760
Reaction score
11,343
Kanisa libadilishe sheria ya Ndoa
Na Mwandishi Wetu-

WANAWAKE wa kanisa katoliki wamedaiwa kutoziheshimu ndoa zao kwa kutambua kuwa kanisa haliruhusu talaka.Kufuatia hali hiyo inayodaiwa wanawake kuwanyanyasa wanaume ili kuweka haki sawa katika ndoa za kikristo kanisa limeombwa kubadilisha sheria ili talaka ziweze kutolewa.

Waumini kadhaa wa kanisa katoliki mjini Mbeya waliohojiwa wamedai kuwa wanawake wengi waliolewa hujingiza katika utovu wa nidhamu na kutoheshimu ndoa.

Mwenyekiti wa vijana wa parokia ya Mwanjelwa Grasiano Nziku ameeleza kuwa wanawake wengi hujivunia sheria ya ndoa ya kanisa ambayo hairuhusu talaka.

Akifafanua alisema ingelifaa kanisa lifikirie mabadiliko ya sheria ili kuruhusu talaka pale kanisa litakapothibitisha kuwa kuendelea kwa ndoa kunaweza kuhatarisha usalama mume na mke.Alisema kuwa sheria ya sasa imewafanya wanandoa kutengana bila kibali cha kanisa na kudumu katika maisha nje ya ndoa kwa muda mrefu pasipo sababu.
 
Ili tupate kulinda ndoa za wenzetu!
Hapa lazima andiko lichakachuliwe kwa mara ingine!

Cc Eiyer MaxShimba Izz
 
Last edited by a moderator:
bible have never said you cant divorce your wife, its church policy which as a person you may not obey it so you dont need a permission to divorce from the people or church for that matter.... and there is no SIN in-front of God by divorcing someone!!!! kama yamekushinda muachane tu!!!!
 

Sasa kama unavyosema ndivyo ilivyo!
Iweje hao waumini waombe biblia igeuzwe? Ili kuwepo na talaka?
Ina maana hao ni wendawazimu kupeleka maombi ambayo hayapo??

Hebu nionyeshe kifungu ktk biblia kina ruhusu talaka!
Nasubiri majibu.
 

So! You are telling me that, church can make things as they go along without following bible??
Lets ask our friend frm parokia ya kanda ya ziwa Eiyer ! Is it possible for a church to go against the bible??
 
Last edited by a moderator:
Sasa kama unavyosema ndivyo ilivyo!
Iweje hao waumini waombe biblia igeuzwe? Ili kuwepo na talaka?
Ina maana hao ni wendawazimu kupeleka maombi ambayo hayapo??

Hebu nionyeshe kifungu ktk biblia kina ruhusu talaka!
Nasubiri majibu.

Kwani kinachozuia talaka kipo?
 
Kwa mjibu wa sheria ya ndoa chombo chenye mamlaka ya kutoa talaka ni mahakama pekee,na kunasababu za msingi ambazo lazima zithibitishwe na kujiridhisha kweli kuwa ndoa hiyo haiwezi kurekebishika kabisa (marriage has been broken irreparably).
Kwa hiyo kama mwenzi wa ndoa anakuzingua kiasi hicho nenda baraza la migogoro wataangalia suala lako halafu utaelekezwa kwenda mahakaman kama ikibii,ili upatiwe talaka yako huko umwache yeye aendelee na hamsini zake.
Kanisa mamlaka zake zinzishia tu kufungisha ndoa na wala si dhambi,mana biblia imesema hivi mtu na asimwache mkewe ila kwa sababu ya uzinzi,pamoja na mambo mengine sheria ya ndoa imeainisha kuwa ukimkamta mwanandoa mwenzio ugoni inaweza kuwa sababu ya kumpa talaka
 
Naona ss mnataka kuchakachua biblia. Wapi biblia imeruhusu talaka. Toa kifungu. Pia kuchakachua biblia imetahadharishwa kwenye kitabu cha ufunuo wa Yohana. "Ole wake aondoae au kupunguza neno ndani ya kitabu hiki maana Mungu ata"....... inaendelea. Kwa wakristo labda kwa zinaa tu.
 

soma mathayo 5:31-32
 
mke/mume hutoka kwa Mungu....sasa kama hukumwomba Mungu akupe mke/mume mwema lazima uhangaike sana...'alichounganisha Mungu mwanadamu asitenganishe'
 
Nimesoma mkuu. Sasa unasemaje. Nashukuru kwa kukazia uzi. "Mmesikia imenenwa lakimi mimi nasema...... ila kwa zina". Na ndo nilivyosema mimi. Labda hukusoma hadi mwisho
 
Kwani kinachozuia talaka kipo?

Soma hapa chini. Biblia inakata katakata kutoa talaka! na ATOAE TALAKA ANA LAANA KWA MUNGU!

By divorcing his wife, the husband puts her in the position where she is strongly tempted to remarry and if she does remarry, Jesus says she is guilty of adultery and so is the man she marries (in contrast to the Mosaic Law which tolerated the remarriage). Hence, the divorce itself is wrong and should be avoided. [Cf. Matt. 18:6,7]

Romans 7:2,3

A married woman is bound by law to her husband as long as he lives. This means that if she is married to another man while her first husband is alive, she is guilty of adultery. She is free to remarry without guilt only if her husband is dead.(Some ask what "law" is this that joins the man and woman - God's law or man's law? It is the law which, when violated, makes the woman an-adulteress. Clearly this must be God's law, and this conforms to what is taught elsewhere.)

1 Corinthians 7:10,11

A married woman should not depart from her husband nor he from her. Again, divorce itself is not the will of God.

Sasa kama andiko linakulazimisha uishi na mwanamke asie na adabu mpaka kufa!!
TUKIMBILIE WAPI??? kwanini mungu wa biblia ana upendeleo!??
 
Mkuu Mungu anasema anakuchukia kuachana! ila biblia imeruhusu kuachana tu pale mmojawapo ya wana ndoa atazini nje ya ndoa. Maandiko hayabadiliki na yatabaki hivyo! Kama vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu vinahusisha uzinzi basi hapo wanaweza achana kama hawataweza kukaa katika meza ya maelewano. Not otherwise!
 

mkuu umefunga mjadala tayari anayetaka bisha aendelee tu!
 
Matthew 19 [:3-9].
when the Jews asked him whether a husband might divorce his wife for any reason, he answered, "'Have you not read that he who made them from the beginning made them male and female, and said, "For this reason a man shall leave his father and mother and be joined to his wife, and the two shall become one"? what therefore God has joined together, let no man put asunder.'

They said to him, ‘Why then did Moses command one to give a certificate of divorce, and to put her away?' He said to them, 'For your hardness of heart Moses allowed you to divorce your wives, but from the beginning it was not so. And I say to you: whoever divorces his wife, except for unchastity, and marries another, commits adultery; and he who marries a divorced woman commits adultery.'"
Source Martin Luther, "The Estate of Marriage" (1522)
 

Sasa hapo ndipo maisha yanaweza kugeuka kuwa balaa!
We chukulia mke au mume SI MZINIFU!
lkn ni mlevi, mgomvi. Matusi na kashfa ndio nyimbo zake!, mharibifu wa mali ya wanandoa! Na mtumiaji wa madawa ya kulevya!
Huyu kwa mujibu wa andiko huwezi kumpa talaka!

Sasa hii kama sio balaa ni nini??
 
mke/mume hutoka kwa Mungu....sasa kama hukumwomba Mungu akupe mke/mume mwema lazima uhangaike sana...'alichounganisha Mungu mwanadamu asitenganishe'

Teh teh teh teh!.
Hapo anti umenisababisha nicheke kwa sana!
Jirani yangu mke wake ana tabia mbaya sana! Inaonekana wakati anaomba mke mwema !dua yake haikufika popote!
 
soma mathayo 5:31-32

Matayo 5:31-32

-“Pia mliambiwa kwamba, ‘Mtu ye yote anayemwacha mkewe ampe talaka.’-32-Lakini mimi nawaambia, ye yote atakayempa mkewe talaka isipokuwa kwa kosa la UASHERATI, anamfanya mkewe mzinzi. Na ye yote atakayemwoa mwanamke aliyepewa talaka ANAZINI.”

Sasa hapa tunaona kuwa, andiko linasema mbali na "UASHERATI" Huruhusiwi kumpa mke au mume talaka!
Hata kama atakuwa MLEVI. MWIZI . MVUTA BANGI . MLA UNGA NA MGOMVI NA MTUKANAJI. NA HATA KAMA ANAMALIZA MALI YOTE KWENYE ULEVI NA STAREHE ZAKE BINAFSI!!

Sasa hapo kazi ni kwa waumini!!

UNLESS WATU WACHAKACHUE BIBLIA!
HAPA NI BALAA KUBWA NDANI ZA NDOA!
Ndio maana wanawake wengi wanafanya kusudi! Kwa kujua andiko linawabeba!!

Heti we Eiyer unasemaje kuhusu hili andiko!
Linahitaji kuchakachuliwa au tumezeee tu! Hata kama mke analewa gongo za pale mabatini. Mwanza!
 
Last edited by a moderator:

mkuu Mbokaleo unasema kweli hayo ni mambo magumu sana ila mimi nasimamia neno la Mungu linasemaje kwa habari ya kuachana. Wengine wanaweza kuwa wamezini lakini wakasameaana maisha yakaendelea. Unajua shida kubwa katika mfano wako hapo ni pale wanandoa wote hawamjui Mungu na hawajui kuwa kwa Mungu kuna msaada MAANA MAANDIKO YANASEMA KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA.Mwanandoa mmojawapo kwa msaada wa Mungu na kwa maombi anaweza mrejeza mwenza wake anayepitia matatizo uliyoyataja hapo juu NDO MAANA YESU ALIKUFA MSALABANI MKUU! NA KWA AJILI YA MAMBO HAYO YESU ALIKUJA DUNIANI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…