Sheria ya Tanzania inaruhusu kuwa na wanajeshi binafsi ‘mercenaries'?

coscated

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
3,264
Reaction score
2,676
Nimekua nikitizama movie series za kimarekani (mathalani ukichukulia mfano movie kama 24 ya Kieffer Sutherland almaarufu Jack Bauer, au Shooter ya Bob Lee Swagger).

Unakuta kuna kikundi flani cha raia ambao wanakua wamepewa mafunzo ya kijeshi na wanakodiwa kwa ajili ya kutimiza mission tofauti tofauti za kijeshi na wanalipwa kwa kazi hiyo.

Je Tanzania tuna sheria inayoruhusu mtu kumiliki kikundi na kukipatia mafunzo ya kijeshi? Na kama hatuna je wanajeshi wetu wanapoenda nchi nyingine (mfano wakati ule wa ukombozi wa nchi za kusini) wanahesabika kama mercenaries(wanajeshi wa kukodi)?

Wajuzi wa mambo naomba mje mnisaidie ufahamu juu ya hili.

Cc Infantry Soldier
 
Alikuwepo scorpion ameshakamatwa
 
Hata hatuitaji hao mercenaries maana ukiwazingua kama malipo au anything afu wako highly trained and efficiently unafikiri kuna kutafuta haki court wao wanaingia front wanachukua nchi .....
 
Ili kufikia kupata makampuni binafsi ya ulinzi kama Black Water na Wagner Brothers Group inabidi sana nchi iwe imeendelea na mifumo yake ya ulinzi iwe imara kinyume chake ni majanga!..
Hayo mambo tuwaachie South Africa wale kidogo wameendelea kuweza kuwa na vikosi binafsi kama anavyokodi Buhari Nigeria!.
 
Tanzania katiba hairuhusu japo vyama vya siasa vinamiliki wanamgambo wanaoitwa walinzi binafsi wa vyama kama Green guard, Red brigade na Blue guard kumbuka lakini hawa hawajasajiliwa kama kampuni binafsi za Ulinzi ( Mfano KK Security na nyinginezo) maana wanalinda viongozi wa vyama tu.
 
Mercenaries unaweza wakodi toka nchi nyingine
 
Ili kufikia kupata makampuni binafsi ya ulinzi kama Black Water na Wagner Brothers Group inabidi sana nchi iwe imeendelea na mifumo yake ya ulinzi iwe imara kinyume chake ni majanga!..
Hayo mambo tuwaachie South Africa wale kidogo wameendelea kuweza kuwa na vikosi binafsi kama anavyokodi Buhari Nigeria!.
Mkuu kama hutojali naomba ufafanuzi zaidi kuhusu buhari na hao wanajeshi
 
Raisi Goodluck Jonathan alipoona majeshi yake yanapigwa sana na Boko haram akaenda South Africa kukodi Specialized Tasks, Training, Equipment and Protection (STTEP) hawa ni mercenaries wa kukodi toka SA.
Buhari alipoingia akaanza kampeni kuwatoa ila kipigo cha Boko Haram kipo palepale!.
 
Panya road, mbwamwitu(mbagala),komando yosso(miaka ya tisini hivi) na wakorea weusi(mbeya).
 
Tanzania hakuna hayo sijui mamercenaries, hairuhusiwi kutoa mafunzo ya kijeshi kwa kikundi binafsi bila idhini ya serikali vinginevyo itahesabika ni uhalifu.
Tena ni uhaini kabisa
 
Back
Top Bottom