Sheria ya ubakaji hasa kwa watoto walio chini ya miaka mitano

Tetty

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Posts
26,355
Reaction score
21,411
Ninaishi kwenye mazingira ya kijijini na kuna incidence imetokea na kwa maelezo ya jamii niliyonayo wanaona kwa mtoto au mtu mzima kubakwa ni kitendo cha aibu na kwenye jumuia hii mtoto/binti anatengwa na kuonekana hafai na ili kuficha siri wazazi wa muadhirika na kijana/mwanaume aliyebaka wanaongea ili kuelewana.Na kiasi anachotoa hakizidi hata laki moja.
Tatizo lingine vitengo ambavyo vinatakiwa kusaidia familia ya mtoto aliyebakwa vinamwacha peke yake na mwisho wa siku mtuhumiwa kuachiwa bila hata kufikishwa mahakamani .Vitengo nina maana polisi,serikali ya mtaa na zahanati au kituo cha afya.

Swali langu kwa wanasheri je sheria imekaaje ili kuweza kusaidia jamii ya aina hii na watu walipatwa na msukosuko huu?
Je polisi na hospitali za vitongoji au wilaya wanaelimu ya kutosha kuhusu sensitivity ya ubakaji?

Na hata wakati wa kwenda kumkamata mtuhumiwa polisi waliiachia familia iliyoadhirika kwenda kumkamata kwa kisingizio polisi wapo wachache.

Je ni sahihi kwa nurse au mtumishi wa zahanati au hospitali kumwambia muadhirika hawezi kumtibu kwa sababu ni usiku na arudi kesho yake asubuhi?Na kama kasoro hizi zipo je mahakama inachukuliaje kesi kama hii,kwamba muathirika toka mwanzo alipopeleka kesi polisi na zahanati hakutendewa haki?

Ninaomba wanajamii mnisaidie sababu hakuna kitu kinachoumiza kama mtoto mdogo kubakwa na kupasuliwa sehemu zake za siri bila kupata haki zake za msingi za kimahakama,polisi na jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…