ile sheria ilitungwa kwa jazba na kwa shinikizo la wanharakati amabao kutokana na vuguvugu la ulingo wa beijing (1995) walimchukulia mwanume kuwa mkosaji na mwenye asili ya mkosaji. .......................na kwa kweli toka wakati huo ukisikia maoni ya wanaharakakti yalionyesha aina ya kumlaumu mwanaume kwa kumkandamiza mwanamke kwa kumnyima haki na kuhodhi madaraka ya utawala. .........................mtazamo huu ndio uliopelekea sheria ile ikatungwa kama sehemu ya mkakati wa uwalinda wanawake na watotot wa kikke wapate fursa kadhaa kama vile elimu bila kukatishwa na tamaa na ukatili wa wanajamii wenzao wa jinsia ya kiume. ...................hatua nyingine za klindaa fursa hizi ililkuwa ni pamoja na kuanzisha kikatiba nafasi za upendeleo wa wanawake (affirmative policy/actions) za ubunge, udiwani na nafazi za uongozi na utendaji serikalini na katika mashirika yake..................
haya yalionekana tangu mwanzo waliokuwa na uelewa wa kutosha na waliikosoa tangu wakati huo. sasa utekelezaji wake ndio unaonekana. .........................sio tu haikuzingatia haki za mtoto wa kiume, lakini pia nadiriki kusema kuwa hata haki za wanawake na watoto wa kike hazikuzingatiwa, mfano unapomfunga baba miaka 30 jela, familia yake (ikiwa na mke na hata watoto wengine wa kike) itaishije ikizingatiwa kuwa familia nyingi baba ndiye anayetegemewa kugharimia mkate, masomo, afa nk.... ..............ni sawa na kusema msichana mmoja alindwe kwa gharama ya kuangamiza future ya familia nzima yenye kujumuisha mke (mwanamke) na watoto (wakiwemo wa kike pia.................. adhabu zilizotungwa na seria hizi zilipitiliza maana ya kuadhibu na kuwa ya kukomoa jinsia ya kiume......................