Sheria ya ugaidi...

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,040
Reaction score
7,303
Wataalam wa sheria na wadau kwa ujumla,

Heshima kwenu nyote,

Kufuatia tukio la kulipuka kwa mabomu na kusababisha vifo huko Boston marekani, kuna swali linenijia.

Vijana wanaosemekana kushirikia katika tukio lile ni wawili toka Chechnya.

Tukio hili limenikumbusha kesi ya ugaidi inayowakabili watanzania wawili Lwakatare na Ludovick.

Upande wa utetezi unajitahidi kujenga hoja za kesi hiyo kufutwa kwa kutokutimiza vigezo vya kuwa kesi ya ugaidi na kigezo kinachosemwa ni kwamba wahusika ni wawili tu wakati sheria inataka wawe watatu au zaidi.

Swali, je kigezo hicho cha watu kuwa zaidi ya wawili hakipo katika sheria za Marekani?

Je, kama hakipo katika sheria za nchi yenye uzoefu zaidi wa kudeal na igaidi ni kitu gani kilichotufanya sisi kukiingiza kwenye sheria zatu.

Asanteni kwa ufafanuzi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…