Sheria ya ujenzi wa ghorofa

Afande Nyati

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
2,385
Reaction score
1,414
Habari zenu wakuu.

Kuna mtu anataka kujenga ghorofa ana pesa zake nyingi tu, ila inasemekana kujenga ghorofa inabidi ukope mkopo bank la sivyo serikali itakufuatilia vyanzo vyako vya mapato na ikiwezekana unaweza kujikuta umefilisiwa.

Na huyu mtu hataki kukopa kwa kutotaka riba sababu ni muislamu. Naomba kujuzwa mtu kama huyu anajisaidia vp na je sheria ya hili suala imekaaje?
 
Wanaokopa ni wale wenye vyanzo visivyoeleweka......wanakopa kuzuga....
Kama fedha zake ni safi kwa nini afilisiwe?
 
Sheria inayombana hapa ni kwamba Nyumba kuanzia ghorofa moja lazima ijengwe Kwa kufuata taratibu za ujenzi,hakikisha anapata consultant Wa kudesign Nyumba hiyo (Architect),then apewe engineer Kwa ajili ya kudesign structures za ghorofa hilo,then taratibu za kujenga atazifanya mshauri Wa ujenzi Qs, halo wote wawe wamesajiliwa Na bodi simamiz za taaluma hizo.

zaidi aingie kwenye tovuti ya CRB/ AQRB au ERB unaweza kupata maelezo zaidi.kikubwa ni kua ghorofa sio jengo la kufanyia mzaha kama halijajengwa Kwa kufuata ushauri Wa wataalam...unaweza sababisha maafa ambayo yanazuilika Kwa kufuata taratibu...Na lazima manispaa au harimashauri husika iruhusu ujenzi baada ya kufuata vigezo vyote.
 
Hii ni kuonesha kuwa serikali imeshindwa kukusanya kodi badala yake inapora mali za watu tu.
 
Wengine ni wafugaji na wana maelfu ya ng'ombe sasa watashindwaje kujenga ghorofa la milioni mia tano(mil 500)?
 
Na kwa sheria ipi?.Halafu navojua chombo chenye nguvu ya kufilisi mtu ni mahakama sa sijui viongozi wanaingieje hapa?!!
 
kama ni pesa chafu Ant- money laundering Act
inakumhusu,kuhusu ujenzi land law na land
planning laws za sehemu husika zitampa
mwongozo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…