Sheria ya umiliki wa vitu vyenye ncha kali iangaliwe upya!

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Posts
13,403
Reaction score
12,775
Ni dakika zipatazo Ishirini nipo maeneo ya Kinondoni Manyanya,kuna kijana/early 40 yuko ndani ya piki piki aina ya boxer bila helment,askari wanaotumia pikipiki almaarufu Tigo anamsimamisha kijana...seem alikua anamhoji kwanini alikua anaendesha piki piki bila helment na pili kwanini anaendesha piki piki isiyokua na usajili!

Ghafla upepo unafumua shati la jamaa wa piki piki na bastola ikawa wazi,Police akaiona na kuanza kuhoji,jamaa kaacha piki piki na kuanza kukimbia kwa miguu kuelekea Maeneo ya Kinondoni Studio,na kabla hajafika mbali Bastola ikamdondoka,(askari kaichukua) askari wakawa wanamkimbiza...walipoona wanampoteza wakapiga risasi mbili hewani jamaa akaanguka kwenye mtaro kwa hofu..Punde gari ya police imefika na kumchukua...nadhani wanaelekea Osterbay!

Nitazidi kufatilia kujua ni nani,kwanini alikua anaendesha piki piki isiyokua na usajili,kwanini alipoulizwa umiliki wa silaha alitimua,na mengine...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…