SoC04 Sheria ya usalama barabarani ifanyiwe mabadiliko. Adhabu zinazotolewa na haziwafanyi madereva kuogopa kufanya makosa na kusababisha ajali

SoC04 Sheria ya usalama barabarani ifanyiwe mabadiliko. Adhabu zinazotolewa na haziwafanyi madereva kuogopa kufanya makosa na kusababisha ajali

Tanzania Tuitakayo competition threads

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Sheria zote hapa duniani huwa zinatungwa na Mabunge ili kuleta manufaa kwenye jamii. Hii ikimaanisha kuwa mtu akivunja sheria iliyotungwa na Bunge basi ataweza kujifunza na kuogopa kutenda kosa tena.

Sheria yetu hapa nchini ya usalama barabarani ilitungwa mwaka 1973. Na kwa jinsi taifa letu lilivyopitia mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi na kimaendeleo haina budi kufanyiwa mabadiliko ili kuokoa maisha ya Watanzania ili madereva wawe makini na kuogopa kusababisha ajali.

Mfano Kifungu cha 40 kinazuia na waendesha vyombo vya moto kusababisha ajali na vifo kwa kuendesha gari bila kujali watumiaji wengine kwa na kuhatarisha maisha yao. Kuhatarisha maisha ya watu kunakosababisha ajali ni pamoja mwendo kasi, ulevi na hata kuendesha chombo cha moto kibovu.

Pia kifungu cha 41 kinazuia waendesha vyombo vya moto kusabisha ajali na vifo kwa uzembe. Mfano mtu kuendesha gari huku anaongea na simu.

Kifungu cha 63 cha sheria hii ya usalama barabarai kinatoa aina za adhabu ambazo Dereva wa chombo cha moto atapewa ikiwa atasabisha ajali..

Mfano Dereva wa chombo cha moto akisabisha ajali kwa kuhatarisha maisha ya watu na kusabisha kifo na akashitakiwa chini ya kifungu cha 40 cha sheria hii, atatakiwa kutumikia kifungo kisichopungua miaka miwili na kisizidi miaka mitatu.

Hali kadhalika dereva chombo cha moto akishitakiwa kwa kusabisha ajali kwa uzembe na kushitakiwa chini ya kifungu cha 41 atatakiwa kulipa faini isiyopungua elfu kumi au isiyozidi elfu thelathini. Na kama amejeruhi mtu atalipa fine isiyopungua elfu mbili au isiyozidi elfu ishirini.

Kwa adhabu kama hizi ambazo kwa mwaka 1973 zilikuwa ni kali na ziliogofya waendesha vyombo vya moto kufanya makosa na kusabisha ajali, mwaka huu 2024 zinawez kuwa na tija?

Upo umuhimu wa Bunge kurekebisha sheria hii adhabu ziwe kali kulingana na wakati uliopo. Ajali haziwezi kupungua wakati Dereva anajua akifanya kosa atalipa faini elfu thelathini na kusepa zake
 
Upvote 3
Back
Top Bottom