Sheria ya ushahidi ipoje?

Myhope

Senior Member
Joined
Jul 20, 2017
Posts
154
Reaction score
67
Shahidi ni mtu mwenye sifa zipi mbele ya mahakama? Je mtu aliyefika mahala ambapo tukio lilitokea baada ya siku 1 au wiki 1 anaweza kuwa shahidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemeana na jambo husika kama shuhuda wa tukio mathalani ajali au ugomvi inatakiwa awepo wakatik tukio linatokea lakini kama ni daktari aliyehusika kumtibu majeruhi wa tukio si lazima awe amemtibu siku ya tukio. Kikikubwa kwenye sheria ya ushahidi ni lazima shaidi atoe ushahidi ambao ni direct kwa maana kile alichoshuhudia na wala si kusimuliwa.
 
Kama ni ushahidi wa wizi je?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni ushahidi wa wizi je?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ushahidi wa wizi lazima utolewe na mtu aliekuwepo kwenye tukio,nikimaanisha aliona au alikuwepo wakati wa tukio.
Kutoa ushahidi wa tukio la wiki kama haukuwepo wakati wa tukio iyo itakuwa hearsay evidence ambayo haikubaliki mahakamani. Lakini kama uliona tukio lakini ukatoa ushahidi siku nyingine inakuvalika.
 
Nimekupata vyema sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je shahidi wa kesi ukimwambia aje atoe ushahidi je lazima kuja au hiari yake sheria ikoje tusaidie hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…