Sheria ya ushoga Uganda: Je, Tanzania tuna lipi la kujifunza?

FURUSHI LA CHANJO

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2022
Posts
874
Reaction score
1,080
Baada ya Museven kujazwa moto na wapambe wake, mwaka 2013 aliamua kuja na sheria kali dhidi ya mashoga nchini Uganda kupitia bunge lake ambapo adhabu ya kosa hilo ilikuwa kifungo cha maisha jela.

Bunge liliipitisha sheria haraka haraka, sheria ambayo ilikuwa kali kuliko sheria nyingine yoyote katika ulimwengu huu isipokuwa sheria dhidi ya mauaji na uhaini.

Kwa mbwembwe zote na madaha ya kisiasa, Museven aliipitisha Rasmi sheria hiyo ili kuanza kutumika na kuwatia hatiani wale wote wanaohusika na vitendo vya kishoga nchini humo.

Baada ya siku kadhaa, kuna beberu moja la Ulaya likaibuka likampiga museven mkwara wa kufa mtu pamoja vitisho vikalii vya kumshughulikia kisiasa na kiuchumi endapo hataifuta hiyo sheria.

Museven alinyauka kama jani kavu la mchicha, akafanya janja janja akaifuta sheria kimya kimya akatokomea shimoni. Waganda wakabaki wanajiuliza kulikoni!!

Hili linatufunza nini kama nchi!! Tuna uwezo wa kushughulika na adha ya ushoga?

Ni nani katika nchi ana uwezo wa kuinuka na kupambana na mashoga hadharani kama KANALI YOWERI KAGUTA MUSEVEN?
 
Hii imekaaje
Screenshot_20230304-124606.jpg
 
Je wewe ni shoga hadi ukimbilie kutaka sheria?
 
Wote mnaolilia serikali ndio izuie ushoga ni wapumbavu tu ivi unategemea serikali ije ikusaidie kumlea mtoto wako kwenye maadili na misingi ya dini sana sana itaweka sheria tu lakini mzigo mkubwa ni kwako mlezi kupambana na maadili ya watoto wenu, sasa wew baki kupiga kelele mtandaoni serikali sijui vile utavuna ulichopapanda Linda familia yako kwa kila hali hayo mengine ni extra tu.
 
Ushoga sio tatizo kwa jamii zetu tuna matatizo lukuki katika jamii zetu,pia ushoga ni hiyari ya mtu na ni dhambi kama uzinzi,tupambane kuleta maji safi,umeme wa uhakika,kupunguza mzigo wa magonjwa,huduma bora za kiafya,ajira kwa vijana n.k

Ukiona kiongozi anahangaika na ushoga huyo anatafuta cheap populality kwa maslahi yake ya kisiasa.
 
Huu muziki ni mnene, wapambe wasijaribu kumuingiza rais kingi azungumzie ushoga mabeberu wanamnasa msimamo wake na watajua anaunga mkono au haungi. Wala bunge lisijaribu kuujadili, badala yake ni kuachana nao. Hii ngoma waachiwe viongozi wa dini japo huko nako kibano wanakipata hasa makanisa ambayo yamefungamana na ya nchi zinazoukubali ushoga. Kwa ujumla upepo huu wa ushoga ni kutumia hekima na busara ili kuepukana nao upite
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na Rais hawezi vaa mkenge rahis kiasi hicho, ni upepo tyuuh utapitaaaaa
 
Ushoga sio tatizo kwa jamii zetu tuna matatizo lukuki katika jamii zetu,pia ushoga ni hiyari ya mtu na ni dhambi kama uzinzi,tupambane kuleta maji safi,umeme wa uhakika,kupunguza mzigo wa magonjwa,huduma bora za kiafya,ajira kwa vijana n.k

Ukiona kiongozi anahangaika na ushoga huyo anatafuta cheap populality kwa maslahi yake ya kisiasa.
Kabisaaaaa
 
Kabisa mkuu serikali iweke nguvu kwenye huduma za kijamii dawa hamna huko mahospitalini watu vijijini wanashindwa kuuza mazao barabara mbovu, maji hamna uanze kuhangaika na zambi za mtu mmoja mmoja ni ujinga.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na Rais hawezi vaa mkenge rahis kiasi hicho, ni upepo tyuuh utapitaaaaa
kuna wanasiasa huwa wana michecheto kujadili mambo ya kipuuzi kama ushoga wakati nchi ina mambo mengi ya msingi kujadili, huu upuuzi waachie watu wa mitaani waujadili maana wanaishi na mashoga hayo wabananishane huko huko
 
Wote mnaolilia serikali ndio izuie ushoga ni wapumbavu tu ivi unategemea serikali ije ikusaidie kumlea mtoto wako kwenye maadili na misingi ya dini sana sana itaweka sheria tu lakini mzigo mkubwa ni kwako mlezi kupambana na maadili ya watoto wenu, sasa wew baki kupiga kelele mtandaoni serikali sijui vile utavuna ulichopapanda Linda familia yako kwa kila hali hayo mengine ni extra tu.
Kazi ya serikali ni nini?
 
Duh.
 
Back
Top Bottom