aroo, inategemeana hiyo mali/shamba ni mali ya nani kisheria. kama ni yako binafsi, hauhitaji ruhusa ya mtu mwingine. kama ni mali yako wewe na mkeo, lazima upate consent ya mkeo. usipofanya hivyo hiyo disposition itakuwa void. ni sawa na mnunuzi kaingizwa mjini na ndio hapo mtakaposhikana naye mashati, kama mchaga atakuja na panga. kwa kawaida, mali nyingi kama umeoa mkuu lazima itakuwa yako wewe pamoja na mkeo, hivyo ruhusa ya mkeo inahitajika. watoto si lazima, hiyo siyo mali yao. haujafa bado mzee unataka waanze kutumia urithi hata kabla haujaenda kaburini...hahaha, hata kama umeshawaandikia wills, itakuwa applicable pale utakapokuwa umekufa. na, will yenyewe uzuri wake warithi huwa hawatakiwi kuiona hadi pale utakapokufa ndo siku yao ya kwanza kuiona ulivyowaandikia. nimeongea kwa lugha rahisi, siyo ya kisheria ili uelewe. una swali?
however, watoto wanaweza wakapinga kama watakuwa na akili, wakagundua kuwa, kwa kufanya hivyo utaathiri maslahi yao, ya mama yao au ya kitu chochote kile. inategemea sababu yoyote ile watakayotoa. na hawatakiwi kukukataza home kule, wanatakiwa waende wakaweke pingamizi mahakamani na maelezo ya mahakama kuhusu uhalali na athari za kuuza. wakiwa na sababu inayokubalika, wanaweza wakawini, wakishindwa ndi hivyo tena. ila kwa kifupi, kama ni kwa nia nzuri, na hakuna madhara, we uza tu kama title/hati ya ardhi hiyo ni jina lako peke yako. kama hati ina mkeo, kaka yako au mtu yoyote yule, lazima consent yake mzee.