SHERIA YASEMAJE..?

fite fite

Senior Member
Joined
Feb 27, 2017
Posts
113
Reaction score
94
Wanajamvi naomba mwongozo juu ya hili kisheria.., dadayangu alikuwa ni mfanyakazi wa ofisi moja kubwa jijini dar es salaam, amefanya kazi katika ofisi hiyo ya binafsi kwa muda wa miaka 8 lakkni hiyo kazi alikuwa anaifanya bila mkataba wowote kutoka kwa mwajiri wake, pili hakuwahi kukatiwa bima ya afya wala kuwekewa hela kwenye mifuko ya hifadhi ya kijamii.
Sasa amesimamishwa kazi bila maandishi yeyote takribani wiki mbili sasa, Je afanyaje ili aweze kupata haki zake na kisheria hili lipoje...? Naombeni msaada wenu waungwana tumsaidie huyu dada anapata shida sana. Naomba kuwasilisha wapendwa.
 
Ameachishwa kwa sababu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…