Sheria za barabarani ziwalenge wananchi sio madereva.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nimekulia nchi ambayo kila mtu wakubwa kwa wadogo wanahamu kuwa ni mwiko mwiko mwiko kuvuka kwenye taa za rangi nyekundu na taa ya kijani ni salama salama salama always. Kila mtu kuanzia watoto wadogo wa shule za awali wanafahamu kuwa sehemu pekee ya watu kuvukia barabara ya ni sehemu yenye alama ya pundamilia (zebra cross), hivyo wataitafuta alama hiyo ya zebra hata kama iko umbali kilometa 1 kutoka pale walipo. Hivyo, hakuna siku watoto waliwahi kuona matumizi ya taa za barabarani na zebra cross yakibadilishwa maana na matumizi yake. Hivyo, hata wanapokuwa watu wazima na pengine kuendesha magari yao kama madereva hawawezi pia kubadilisha maana na matumizi ya rangi za taa za barabarani na zebra cross kamwe kamwe kamwe.

Hali hii ni tofauti na hapa Tanzania (Dar es Salaam), watoto wetu hawana cha kujifunza kutoka kwetu na kwa matraffic kuhusu sheria za barabarani kwakuwa sheria zetu zetu za barabarani ni kwa madereva na wamiliki wa magari tu. Kuna wakati magari yanalazimishwa na traffic kupita taa nyekundu na kusimamishwa kwenye taa za kijani, watoto na watu wazima wanaweza kuvuka na kuvushwa barabara kokote na popote bila kupewa adhabu wala kalipio (vuruvuru). Watoto wa aina hii hawawezi kuwa madereva wazuri wanaozingatia alama za barabarani watakapokuwa wakubwa.

Watoto wanafundishwa shuleni alama za barabari lakini wanaporudi mitaani wanakuta na kuona kitu kingine kabisa.

Mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo, tuwafundishe watoto wetu matumizi sahihi ya barabarani, wacha taa na alama za barabarani zifanye kazi yake kwa watu wote kwa wakati wote. Wacha foleni za magari ziongozwe na taa na alama za barabarani na traffic wasimamie wote (waenda kwa miguu, madereva na wamiliki wa vyombo vya moto) wanaozivunja. Watoto wetu watapata cha kujifunza wangali bado wadogo badala ya kutengeneza kizazi kisichoheshimu alama za barabarani eti kisa foleni ndefu za magari, hadi lini???
 
NAULIZA TU...HIVI MADEREVA NAO SIO WANANCHI??

ELIMU NI KWA WATU WOTE MI NIJUAVYO HAMNA KUBAGUA KUNDI FULANI
 
NAULIZA TU...HIVI MADEREVA NAO SIO WANANCHI??

ELIMU NI KWA WATU WOTE MI NIJUAVYO HAMNA KUBAGUA KUNDI FULANI
mungu anakuona, elimu hiyo ingekuwepo usingekuta maua na nyasi vimekanyagwa na watembea kwa miguu
 
Yani umeshindwa kuweka kichwa cha habari vizuri,umeshindwa kujieleza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…