SHERIA ZA BENKI: Zifahamu Kanuni Mpya za kulinda Wateja wa Mabenki na Taasisi za Fedha

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
1608099695045.png

Benki kuu ya Tanzania (BoT) imepitisha kanuni mpya za kulinda wateja wa mabenki na taasisi za kifedha. Kanuni hizo zijulikanazo kama the Bank of Tanzania (Financial Consumer Protection)

Regulations 2019 GN No. 884 of 2019 zimeanza kutumika kuanzia tarehe 22 Novemba 2019. Kwa ujumla, kanuni hizi zinatoa haki na wajibu kwa Mabenki na Taasisi za kifedha katika kulinda haki za wateja wao. Kwa kifupi, kanuni hizi zinaweka matakwa yafuatayo kwa Mabenki na Taasisi za kifedha, ambayo ni pamoja na:-

1. Bodi ya wakurugenzi ya Benki au Taasisi ya kifedha imepewa majukumu ya kusimamia na kuratibu utekelezaji wa sera na taratibu zote zinazohusu haki na ulinzi wa mteja ikiwa ni pamoja na kuratibu menejimenti katika kusimamia utekelezaji wa sera za kumlinda mteja.

2. Benki na taasisi za kifedha zinatakiwa kuwa na sera mahususi inayozungumzia na kuweka bayana taratibu na miongozo ya kumlinda mteja.

3. Kanuni pia zinaweka miongozo ambayo Mabenki na Taasisi za kifedha zinatakiwa kudhibiti kama njia ya kumlinda mteja ambazo ni:-

a. Kutobagua wateja.
b. Kudhibiti vitendo vya kidhalimu vya kibiashara (unfair business practices)
c. Kuzuia njia au taratibu za kudhalilisha za ukusanyaji wa madeni (abusive debt recovery practices).

d. Kusimamia maadili ya kazi na taaluma haswa wakati wa kufanya mauzo ya bidhaa za kibenki.

e. Kuzia kuuza bidhaa ambazo hazieleweki au hazina tija kwa mteja.

f. Kulazimishia mteja kuchukua huduma/bidhaa ambazo zimefungamanishwa pamoja (tying products).

g. Kuongezea au kuhuisha mkopo mpya bila kutoa taarifa na kupata ridhaa ya mteja
h. Kutoa au kuuza bidhaa/huduma sahihi kwa wateja.

i. Kuruhusu wateja kuhama benki/taasisi moja kwenda nyingine bila vikwazo au masharti magumu yasiyotekelezeka.

j. Kuacha kutoa taarifa zisizo za kweli au za kughilibu wakati wa kuuza huduma ili kumfanya mteja ashawishike.

4. Kanuni pia zinazitaka Benki na taasisi za kifedha kutoa taarifa na kuweka bayana mambo yafuatayo:-

a. Kutoa taarifa/kuweka bayana kuhusu bidhaa na huduma zitolewazo na Benki au Taasisi za fedha kwa lugha nyepesi na inayoeleweka.

b. Kutoa taarifa/kuweka bayana kuhusu gharama na tozo mbalimbali zinazotozwa na benki/taasisi za kifedha.

c. Kutoa taarifa/kuweka bayana kuhusu gharama, ada, tozo, rejesho na riba zitokanazo na mikopo.

d. Kutoa taarifa kuhusu njia mbalimbali zinazoweza kusababisha wizi, upotevu au udanganyifu katika fedha za mteja.

e. Kumpatia mteja taarifa kuhusu miamala yake (account statements) kwa kipindi

5. Pia, kanuni zinazitaka Benki na taasisi za fedha kufanya yafuatayo:-

a. Kumrejeshea mteja dhamana (collateral) mara moja baada ya kumaliza mkopo wake tena bila vikwazo au sababu.

b. Kumtaarifu mteja endapo kuna mabadiliko yeyote kuhusu vigezo na masharti yanaohusu bidhaa au huduma.

c. Kuweka mifumo madhubuti ya kuzuia udanganyifu, wizi au upotevu wa fedha za wateja.

d. Kutotoa taarifa za mteja kwa mtu yeyote bila ridhaa ya mteja isipokua tu pale sheria inapotaka taarifa hizo zotolewe.

e. Kutumia lugha au masharti yanaoeleweka kwenye mikataba au taarifa kwa wateja.

f. Kutoa elimu kwa umma au wateja wa Benki/Taasisi ya kifedha haswa katika masuala ya kifedha.

g. Kudhibiti upotevu au wizi wa fedha za mteja. Endapo wizi au upotevu wa fedha za mteja utafanyika basi kurejeshea fedha hizo mara moja.

6. Kanuni pia zinatoa muongozo wa jinsi ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko yatokanayo na kusimamia haki za wateja kama ifuatavyo:-

a. Kanuni zinaitaka kila Benki au Taasisi ya kifedha kuwajibika kuweka mfumo wa kusimamia malalamiko ya wateja wake kwa njia mbalimbali kama vile kupitia, simu, barua pepe au kupitia mitandao.

b. Aidha, kanuni zinampa mteja haki ya kuwasilisha malalamiko yake kwa Benki au
Taasisi ya kifedha na kushughlikiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kumpa mteja mrejesho kuhusu utatuzi wa malalamiko yake.

c. Kwa mujibu wa jedwali la 2 la kanuni husika, kanuni zimetoa muda wa masaa 6 hadi 48 kwa Benki au Taasisi ya kifedha kushughulika malalamiko ya mteja kulingana na aina ya malalamiko. Aidha, kwa zile huduma za kibenki moja kwa moja, kanuni zimetoa muda wa masaa 2 hadi siku 14 kushughulikia malalamiko ya mteja kulingana na aina ya malalamiko.

d. Kanuni zinaruhusu pia mteja kuwasilisha malalamiko yake Benki Kuu endapo hatapata suluhisho au kutoridhika na utatuzi wa malalamiko yake kutoka kwa Benki au Taasisi ya Kifedha.

Endapo mlalamikaji hataridhika na maamuzi ya Benki kuu, Kanuni zinatoa mwanya kwa mlalamikaji kuwasilisha malalamiko Mahakama Kuu.

Uchambuzi huu kwa hisani ya FIN & LAW Advocates
 
Upvote 4

imependezaAAA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona taarifa za kibenki za kakobe zilianikwa wazi kama tangazo la kifo?mabenki ya tanzania hovyo siasa tupu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom