Sheria za biofuels hapa Tz

Mtu Poa 2013

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
105
Reaction score
65
Kuna rafiki yangu ana mpango wa kuanzisha kakiwanda ka kutengeneza mafuta ya diesel kwa kutumia mbegu za Jatropha. Kwa hapa tz nilikuwa sifahamu sheria zinasemaje kuhusu uanzishwaqji wa miradi ya biofuels so nikawapigia wizara ya nishati na ewura, wanasema kumbe hakuna sheria rasmi inayoongoza mambo ya biofuels. Ni siasa tu. Sasa mi nawauliza walioshaanzisha miradi kama hii au ambao wako kwenye process, naombeni experience yenu katika kuanzisha miradi hii. Mlipataje vibali?
 

Mkuu how far did you go with this? nimevuna mibunu mingi sana na nipo kutafuta mtu anaeweza kuchuja mafuta, vp rafiki yako alifanikiwa kuanzisha? na je kuna mtu mwingine unaefaham ana fanya hiz issues?
 
Jaribu kutembelea pale Tatedo wapo Jaribu na chuo cha ustawi wa jamii kijitonyama.
 
nchii hii kila kitu siasa tu kwa kweli,
bio fuel ni dili sana kwa sasa hasa upande wa Jatropha oil
nchi nyingi zimeadvance wanatumia hayo mafuta kutengeneza sabuni, mafuta ya kuendeshea magari hata ndege (za abiria), kutegeneza biogas na hata katika biashara ya carbon credit, mimi nimefanya hiyo miradi na wadutch Kilimanjaro, lakini tulipokuwa tunataka kuexpand mradi wetu, serikali ikatujia juu, so ni blabla tu.. lakini kenya wamepiga hatua kuna kampuni jina limenitoka wanataka itakapofika by 2015 zaidi ya 90% ya public car ziwe zinatumia hayo mafuta ni mafuta economical sana .. kwa mfano kama disel au petrol unatumia lita 1 kwa 10km basi kwa jatropha oil unaweza kwenda hata 13 km kwa lita hiyo moja.

Kuna wamama wakimasai walikuwa hapo umasaini arusha walianzisha vikundi vya kutengeza sabuni za jatropha na wakawa wanawauzia wazungu wanaoenda kutalii mbugani.. nawalikuwa wanapiga sana pesa, gafla serikali iakwazuai.. mara hawana leseni, mara waenfde tbs mara tfda , mara wajisajiri yaani ni full longolongo..

Kila lakheri kwa huyo madau anayetaka kujaribu, lakini kama serikali ingeweka mazingira ya kuwafinance wazawa na vijana na kuweka fursa vizuri Jatropha ni big deal, kwanza halina gharama kama any horticulture crop, labda kwa magonjwa kidogo.. but yanatibika.. na bado unaweza fanya kilimo mseto yaani kumix jatropha with food crops na ukavuna ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…