babumangindo
New Member
- Mar 8, 2011
- 1
- 0
Kumfukuza mwanafunzi masomo moja kwa moja kwa kufeli somo moja,au kwa kufanya udanganyifu katika somo moja ni halali?kama ndiyo haki ya mtu kupata elimu ipo wapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hakuna remedy yoyote kama chuo chako kina sheria na kati ya hayo uliyoyaelezwa yamekatazwa na sheria hiyo na kama idhabu iliyotolewa imeainishwa na sheria na kaba ulifanyiwa fair trial na ukapewa haki zako zote za asili na ukapatikana na hatia.Haki ya kupata elimu ni kwa mtu anayekuwa tayari kuipata elimu hiyo ikiwepo uwezo wa kuyaelewa masomo kwa ngazi uliyoiomba.kama wewe ulistahili kupata cheti alafu ukakimbilia kwenye shahada na wakati ubongo wako haujai hata kwenye kijiko na unaanza kufanya udanganyifu ili uvune usicho kipanda ulitarajia chuo kikufanyeje?ulitarajia ungemaliza chuo kwa staili hiyo ungefanya kazi gani?au ni chuo gani kinapenda kuona wahitimu wake ni vihiyo na hawatoi output nzuri kwenye soko la ajira?acha udanganyifu soma kwa bidii utafanikiwa.inaonekana hata kenye elimu za chini ulikuwa unafanya udanganyifu sasa umekwaa kisiki.elimu pekee ambayo ni haki isiyo na wajibu ni elimu ya msingi lakini kuanzia sekondari na kuendelea kuna wajibu wa kusoma na kuyaelewa masomoKumfukuza mwanafunzi masomo moja kwa moja kwa kufeli somo moja,au kwa kufanya udanganyifu katika somo moja ni halali?kama ndiyo haki ya mtu kupata elimu ipo wapi?