Imekuwa ni tatizo na gumzo la kila siku katika vyombo vya usafiri, majukwaa ya kisiasa, mitaani, katika maeneo ya biashara, kumbi za starehe, maeneo ya michezo, mashuleni na katika vyuo. gumzo lenyewe linahusiana na hatua za kusimama toka ilipo kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura. Jana, 14.10.2015 nilikuwa katika basi moja la abiria nasafiri kutoka Arusha kuelekea Dsm. Nikiwa kwenye basi hilo, abiria walianza kujadili ukweli kuhusu hatua hizo. katika kuchuja mawazo yao, niliweza kujua kuwa wengi wao wanajua ni mita mia moja. Ili kuondoa utata huu, Je sheria inasemaje? siku moja nilimsikia mwanasheria mmoja katika mdahalo akisema, sheria inasema mita 200 na wala haitamki mita 100. sasa hii mita 100 inatoka au watu wameitoa wapi? tuachana na hilo, sote tusome sheria hiyo ya uchaguzi tujionee ni mita 100 au 200. tuache kulumbana pasipo kujua. Na kama ndivyo, kuna vituo vingine huwezi kupata hizo mita hata 100. je tusimame wapi? ni vyema tuutafute huo ukweli ili ukweli huo utuweke huru.