Sheria za Uhamiaji zibadilishwe na taratibu za kushikilia nyaraka zibadilishwe

Sheria za Uhamiaji zibadilishwe na taratibu za kushikilia nyaraka zibadilishwe

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Mengi sana yamekuwa kama kandamizi, kukiuka haki za binadamu pia zikiwapa mamlaka makubwa ma afisa uhamiaji kujiona kama vile wao ndio miungu watu na waogopwe, kwa mfano:

1. Unaambiwa kwamba Kitambulisho cha taifa hakiwezi kukuhakikishia Uraia: sasa ninapo jaza fomu, kuwasilisha nyaraka na mwenyekiti wa mtaa au kijiji kuni sainia fomu yeye akiwa yuko na mimi kwenye eneo lake akiwa ananifahamu vizuri kunawezaje kutonipa uhalali wa kuwa raia. Hii ina tafsiri kuwa ma afisa uhamiaji wanasema hatuna kitambulisho chochote nchini kinachoweza kutambulisha uraia wetuhata passport bado haijatupa uhalali (kwamba hata kama unavyo lazima uhojiwe kwa kina sana) bali wao tu ndio wenye mamlaka ya kusema wewe sio raia au ni raia basi.

2. Swala la uchunguzi wa uraia wa mtu usio kuwa na kikomo: watu wengi wamekuwa kwenye detention ya kifungo cha nje hata kama itazidi miaka 20 unaambiwa uchunguzi wa uraia wako bado unaendelea au ni endelevu, sasa hawa ma afisa kazi yao ni nini, kwani uchunguzi hauwezi kuchukua miezi 5 au 6 na ikawa concluded? wanaichukua pasi yako wanakaa nayo kwa muda wautakao wao. huu ni ukoloni, huu ni unyanyasaji.

3. Wengi wametokea Bukoba, Kigoma mipakani kabisa wanajiona wao tu ndio raia wa nchi hii wakati tunafahamu fika kule kuna muingiliano sana tu na Waburundi, Waganda na Rwanda sasa ukimuuliza yeye athibitishe kama hana mchanganyiko wa nchi zile anakuona adui anaanza kukuchunguza wewe na kukuchukua maelezo kwani wao ni kina nani nao hawawezi kuhojiwa na sisi raia wa kawaida kuhusu uraia wao. Wao kuwa ma afisa uhamiaji hakuhalalishi moja kwa moja kuwa lazima ni raia 100%

Najua watauchukia uzi huu ila wakubali tu yaishe na wabadili sheria zao ili tukae nchini kwetu kwa amani bila manyanyaso na sheria kandamizi na za kikoloni.
 
Raisi Samia aruhusu tu Uraia pacha, siasa za Uswahilini ambazo bado zinaogopa Makabaila na Mabwanyenye Makaburu na Mabeberu zimeshapitwa na wakati
 
Kama huna cha kuchangia usiharibu uzi
Hujui kitu dogo
Izo akili za ki M4c zinawadumaza sana upeo wenu wa kufikiri, fikra chanya.
Kwa akili yako kinyesi unaona uraia pacha Ni salama kwa taifa letu?
 
Back
Top Bottom