Sheria zote nchini kuwa kwa Kiswahili

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome amesema kuanzia sasa sheria zote zitakazotungwa nchini zitakuwa katika lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi ambao ndio walengwa wa sheria hizo, kuzielewa.

Uamuzi huo unakwenda sambamba na kuzitafsiri sheria zote zinazotumika nchini ambazo ziko katika lugha ya Kiingereza ili kutimiza lengo hilo la kuwafanya wananchi wengi wazielewe.

“Kwa sasa serikali imeamua kuwa sheria zote nchini zitakuwa katika lugha ya Kiswahili na zile ambazo ziko katika lugha ya Kiingereza zitatafsiriwa ili kuwawezesha Watanzania wengi ambao ndio walengwa wa sheria hizo kuzielewa,” alisema.

Pia alisema serikali itazifanyia marekebisho sheria zote ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wadau mbalimbali kuwa hazikidhi mahitaji au haja, haziendani na wakati uliopo sasa ili kutekeleza azma yake ya kuwahudumia wananchi wake kwa ukamilifu.

Profesa Mchome ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana baada ya kupokea mapendekezo yaliyowasilishwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WILDAF), ambayo yanataka kufutwa kwa sheria mbalimbali za kimila zinazosimamia masuala ya mirathi ambazo zinalalamikiwa kuwakandamiza wanawake nchini.

Profesa Mchome amewashukuru WILDAF kwa kazi waliyoifanya na kuwaahidi kuwa wataalamu wake wizarani watayafanyia kazi mapendekezo yao ili kuhakikisha gurudumu la sheria nchini linasonga mbele na kuwasaidia wananchi wengi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa WILDAF, Judith Odunga alisema mapendekezo hayo yanataka kufutwa kwa sheria za kimila ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwakandamiza wanawake, kuwanyima haki ya kumiliki mali na kufanyiwa vitendo vya kidhalilishaji pale wanapofiwa na waume zao.

Alisema katika mapendekezo hayo WILDAF inaiomba serikali itunge sheria moja ambayo pamoja na zile za kidini itashughulikia masuala ya mirathi na kuweka usawa wa kisheria katika urithi wa mali kati ya mwanamke na mwanamume, ikiwa ni pamoja na watoto wa kiume na wa kike kuwa na usawa katika kurithi mali inapotokea mzazi wa kiume amefariki dunia.

Chanzo: HabariLeo

Habari hii imesomwa pia kwenye kipindi cha JAMII LEO..

Nzuri sana hiyo,wengi wapo jela kwakuwa walishindwa kuelewa stahili zao katika sheria na sio kuwa walikuwa na makosa ya kusababisha kuwa jela miaka 2 mpaka 3

Watu wanetukanana na jilani yake kisha mtu anaenda kuwekwa Segerea mahabusu miaka mwezi 6, atii upelelezi unaendelea, jamani hata hilo kumbe ni tatizo la muhusika kutojua haki yake tu kwa sababu ya lugha ya kigeni, kama serikali imeliona hilo itakuwa njema sana ,
 
Sheria zote Nchini kuwa kwa Kiswahili

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome amesema kuanzia sasa sheria zote zitakazotungwa nchini zitakuwa katika lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi ambao ndio walengwa wa sheria hizo, kuzielewa.

Uamuzi huo unakwenda sambamba na kuzitafsiri sheria zote zinazotumika nchini ambazo ziko katika lugha ya Kiingereza ili kutimiza lengo hilo la kuwafanya wananchi wengi wazielewe.

“Kwa sasa serikali imeamua kuwa sheria zote nchini zitakuwa katika lugha ya Kiswahili na zile ambazo ziko katika lugha ya Kiingereza zitatafsiriwa ili kuwawezesha Watanzania wengi ambao ndio walengwa wa sheria hizo kuzielewa,” alisema.

Pia alisema serikali itazifanyia marekebisho sheria zote ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wadau mbalimbali kuwa hazikidhi mahitaji au haja, haziendani na wakati uliopo sasa ili kutekeleza azma yake ya kuwahudumia wananchi wake kwa ukamilifu.

Profesa Mchome ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana baada ya kupokea mapendekezo yaliyowasilishwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WILDAF), ambayo yanataka kufutwa kwa sheria mbalimbali za kimila zinazosimamia masuala ya mirathi ambazo zinalalamikiwa kuwakandamiza wanawake nchini.

Profesa Mchome amewashukuru WILDAF kwa kazi waliyoifanya na kuwaahidi kuwa wataalamu wake wizarani watayafanyia kazi mapendekezo yao ili kuhakikisha gurudumu la sheria nchini linasonga mbele na kuwasaidia wananchi wengi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa WILDAF, Judith Odunga alisema mapendekezo hayo yanataka kufutwa kwa sheria za kimila ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwakandamiza wanawake, kuwanyima haki ya kumiliki mali na kufanyiwa vitendo vya kidhalilishaji pale wanapofiwa na waume zao.

Alisema katika mapendekezo hayo WILDAF inaiomba serikali itunge sheria moja ambayo pamoja na zile za kidini itashughulikia masuala ya mirathi na kuweka usawa wa kisheria katika urithi wa mali kati ya mwanamke na mwanamume, ikiwa ni pamoja na watoto wa kiume na wa kike kuwa na usawa katika kurithi mali inapotokea mzazi wa kiume amefariki dunia.

My Take
Ni jambo la kupongezwa.
 
Na mahakamani, patakua je, hukumu zitaandikwa kwa kiswahili au?
Vipi kuhusu wanafunzi wanaosomea sheria, mitihani itakua kwa kiswahili pia?
 
Duh!! Hizi propaganda hizi .... na sheria wafundishwe kwa Kiswahili!!
 
Nimewahi kukutana na Prof huyu katika forums tofauti, lakini niseme tu sijawahi kuona "competence" yake na hasa kwenye masuala ya kiuongozi. Huwa anatumia majibu rahisi kujibu maswali magumu. Alipokuwa Katibu Mkuu wa Elimu, aliposhindwa kuifanya elimu iwe shindani na kuzalisha vijana wenye uwezo, na wanaoweza kupasi mitihani, solution alioiona ni kubadilidha mfumo wa alama na kupunguza pass mark pamoja na GPA system. Badala ya kujibu swali gumu kwanini watanzania walio wengi wamashindwa kuielewa lugha ya kiingereza na hivyo kunufaika na fursa za lugha hiyo duniani ikiwa pamoja na kujua sheria zilizoandikwa kiingereza, amekuja na majibu rahisi tena ya kubadilisha lugha iliyotumika kuandika sheria. Sasa nasubiri, je watakapoziandika kwa lugha ya kiswahili na kisha kubaini watu wengi wanaelewa zaidi zikiwa kwenye lugha zao za kimakabila, sijui atakuja na mkakati wa kuziandika sheria katika lugha za kimakabila?

Nchi zote za kiafrika zinatumia Lugha tatu tu katika masuala yao makubwa (ama kuendesha Serikali au mfumo wa Elimu). Bahati nzuri Lugha zote hizo tatu ni za Kimataifa (English, French and Arabic). Si kwamba hawana lugha zao za ndani, bali wamebaini lugha zao si shindani hivyo zitawatoa katika ulingo wa kimataifa. Unfortunately, nchi yetu ndio inataka kuelekea huko. Tunakipenda sana kiswahili, na ni fahari, lakini hakina utayari wa kuipeleka nchi katika Uchumi wa kati. Tukomae kwenye kujua kiingereza kina nafasi sana katika dunia ya leo kuliko kiswahili. Tusidanganyane jamani.
 
Hili lilitarajiwa kwa maana nasikia mkuu wa kaya hawezi hata kitenzi kwa kiingereza kinaitwaje.
 
Sidhani kama ni sahihi kufanya hivyo. Maana huko vyuoni wanafundisha kingereza kutokana na kwamba vitabu vyote vya sheria kuandikwa kwa kingereza Lugha mama ya Taifa ambalo tumekopi sheria zake zote.
 
Mimi nitazisoma zilezile za kiingereza nilizozizoea , Sikubaliani na Sifuni Mchome hata kidogo , ikumbukwe kwamba huyu ndiye aliyeleta DIV 5 akishirikiana na Shukuru Kawambwa na Phillipo Mulugo .
 
Sina imani tena na ma-prof wa kitanzania ukiacha wa SUA!!
 
Sidhani kama ni sahihi kufanya hivyo. Maana huko vyuoni wanafundisha kingereza kutokana na kwamba vitabu vyote vya sheria kuandikwa kwa kingereza Lugha mama ya Taifa ambalo tumekopi sheria zake zote.
Ni raha sana kuwa na watumishi serikalini wasioweza ngeli ya malkia!
 
Mkuu nimekupata, naona nchi yetu inakazana kuwa Korea ya Kaskazini. Lengo ni kuwakomoa waliopeleka watoto English Medium Schools na nje ya nchi. Nchi kila kukicha kubadili pazuri tuliyorithi badala ya kuyakuza Na kuyaendeleza. Kuna ubaya gani kupromote English kama lugha ya kusoma kwa kuwa vitabu vingi Na taarifa vimeandikwa kwa English? Leo hii utamfundisha Medical Doctor terminology za medicine kwa Kiswahili?
 
Kama umeshindwa kulielewa suala rahisi kama hili linalohusu sheria kutafsiriwa kwa lugha ambayo wananchi wanaielewa sishangai kishindwa kumuelewa Profesa katika yaliyo magumu zaidi.
Hakuna marufuku ya kuandika sheria kwa kiingereza lajini sasa kutakuwa na fasiri ya swahili kwa sheria zote hili lina ugumu gani?
 
Ndugu usinitoe akili labda hujaelewa kinachojadiliwa. Hapa kuna mambo mawili: kutafasri sheria na lugha inayotumika kuandika sheria. Hakuna mwenye tatizo na kutafsri sheria kuwa katika kiswahili kwani hilo limekuwa likifanyika toka awamu ya Rais wa Kwanza. Sort of discussion hapa ni Lugha ya sheria. Sina miwani na utandu wa kutoelewa maandishi mkuu.

“Kwa sasa serikali imeamua kuwa sheria zote nchini zitakuwa katika lugha ya Kiswahili na zile ambazo ziko katika lugha ya Kiingereza zitatafsiriwa ili kuwawezesha Watanzania wengi ambao ndio walengwa wa sheria hizo kuzielewa,” alisema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…