Shetani yupo kwenye kampeni

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
Imeandaliwa na kuandikwa na Dogoli kinyamkela

Leo nilikuwa nausikiliza wimbo ya Bahati bukuku KAMPENI, na humo ndani anasema kwamba shetani Yuko kwenye kampeni.

Hajakosea Ni kweli shetani Yuko kwenye kampeni lakini je katika hiyo kampeni anashindana na Nani?

Hapa jibu Wala halihitaji elimu ya chuo moja kwa moja tutajibu kwamba kampeni dhidi ya yuleee ambaye tunaamini au tunamuita Mungu.

Je kampeni ya shetani inafanywa au inasimamiwa na Nani, na je kampeni ya upande mwingine ambao tunaamini Kama ndiyo upande wa Mungu nayo inafanywa au inasimamiwa na Nani?

Kwenye kampeni Kuna kuwa na vibaraka lakini mwisho wa siku muhusika mwenyewe ndiyo inatakiwa aingie jukwaani na kujiombea kura mwenyewe, je wewe katika kampeni hii ya pande hizi mbili umekutana na vibaraka au umekutana na wahusika wenyewe?.

Lakini kingine Kati ya wapiga Kura na mpigiwa Kura au mgombea Ni Nani mwenye nguvu? hapa jibu Ni rahisi tu kwamba mpiga Kura ndiyo Ana nguvu japo ajijui, yaani mpiga Kura ndiyo anayempa nguvu Yule mgombea.

Tuanze Sasa, Kama shetani kwenye kampeni zake mshindani wake Ni Mungu Basi shetani na Mungu wametoka katika chanzo kinachofanana, na lengo lao wote Ni moja, kutawala.

Kila chama kinapomsimamisha mgombea huwa kunakuwa na Sera zake, au kila mgombea anakuwa na Sera zake.

Naam sote twajua kwamba Sera za shetani asilimia kubwa Ni uovu na hata Kama Ni wema Basi mwisho wake huwa tunaamini hautakuwa mzuri.

Na Sera za Mungu tunaamini kwamba Ni wema au uzuri.

Lakini asilimia kubwa hizi Sera tumekuwa tukizisikia kutoka kwa vibaraka wa hizi pande mbili, japo vibaraka hao hao kunawakati wanatangaza wema huku wao wakishindwa kuufanya huo wema.

Vibaraka Ni wengi Sana, mfano wa vibaraka hao Ni serikali, viongozi wa dini, baadhi ya watu mashuhuri nk.

Lakini swali lingine la kujiuliza wao wameteuliwa na Nani kuwa vibaraka, na je muhusika mwenyewe yu wapi?

Kwa wake ambao wamekuwa wakisafiri kwenye dimensions tofauti tofauti, Wenda Kuna sehemu ambayo watakuwa wamefika.

Na hiyo sehemu Kama usipokuwa makini Basi utaishia kuwa kibaraka, lakini kibaraka aliyepata mamlaka kutoka kwa mgombea husika.

Vibaraka wengi Ni wale vibaraka wa Imani kwamba nimezaliwa katika Imani Fulani nami naendelea kufundisha hiyo Imani, lakini Kuna vibaraka ambao hao wamekutana kabisa na huyu shetani au huyu tunayemuita Kama Mungu.

Natamani kila mtu afike hapo kwa Hawa wahusika wawili wakiwa wanafanya kampeni zao, yaani uwaone live hivi, uzuri katika kampeni zao Wala hawafanyi kila mtu kwa wakati wake Ila wote wanafanya kwa wakati mmoja na sehemu moja.

Hivyo katika kampeni zao unakutana nao wote wawili kwa wakati mmoja, na kila mmoja anachoomba Ni wewe umchague yeye.

Yaani shetani anaomba umchague yeye, na huku Mungu pia akiomba umchague yeye.

Hapo wewe unakuwa na chaguo Sasa uondoke na Nani Kati ya hao wawili.

Na kama unavyojua siku zote mpiga Kura ndiyo mwenye nguvu Ila kabla hajaipiga Kura yake, Ila akishapiga Kura tu pale anakuwa ameiuza nguvu yake au nguvu zake kwa Yule aliyemchagua.

Hivyo wote wapo kwenye kampeni ili waendelee kuwa na nguvu katika ulimwengu huu wa matrix.

Kama ukimchagua shetani hapa utakuwa mnyama, katili, lakini katika kila utakachokifanya Ni kwa ajili ya kukunufaisha wewe, yaani utakuwa katili kwa sababu ya manufaa yako wewe mwenyewe.

Na Kama ukisema umchague Mungu utakuwa mwema kwa wengine Hali ambayo itapelekea wewe uumie Sana kwa ajili ya wengine na yote hiyo Ni kwa sababu ya huo wema wako.

Lakini je vipi Kama usipompigia kura yeyote Yule Kati ya hao wawili.

Kama usipompigia kura yeyote Kati ya hao Basi wote wawili wataingia ndani yako, na hapo utakuwa umeuvunja mnyororo huu wa matrix, yaani hapo utakuwa umeweza kuunganisha mbili ikawa moja.

Hapo wewe ndiyo utakuwa yuleee mwenye kuiumba Nuru na kulihuluku Giza, wote wale watakuwa ndani yako kukutumikia na Wala si wewe kuwatumikia.

Hapo Sasa utakuwa umeunganishwa na kila kitu, na utaweza kushuhudia live kwamba wewe Ni vyote, maana hapa Sasa hata ukilichuma Jani Kama Ni maumivu ya Jani Basi wewe ndiyo utayasikia.

Na Kama ukigusa chochote Ile kusensi kwa kitu au ule mpapaso Ni wewe ndiyo utayasikia, na hata Kama ukimpiga mwingine Basi Ni wewe ndiyo utaumia.

MUNGU wa kweli yeye Ni kila kitu, yaani vyote vimetoka kwake, Wala Hana muda wa kufanya kampeni au kujielezea kwa sababu anajua yeye Ni kila kitu na kila kitu Ni yeye.

Wewe ndiyo mmili wa funguo za mlango wako, lakini siyo funguo inayomfungua mlango Ila Ni wewe ndiyo ufunguao mlango.

Ulikuwa nami mwalimu wako Dogoli kinyamkela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…