Shetta aeleza jinsi alivyonusurika kwenye ajali mbaya aliyoipata juzi

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304

Rapper Shetta alipata ajali mbaya ya gari wakati akielekea Babati, mkoani Manyara kufanya show, lakini Mungu alimnusuru yeye na watu wengine wawili aliokuwa nao katika gari hilo.

Akiongea na Times 100.5 Fm, rapper huyo amesimulia jinsi ajali hiyo ilivyotokea ambapo ametaja chanzo cha ajali hiyo ni kumkwepa pundamilia aliyekuwa akikatiza barabarani.

“Mi nilikuwa natoka Dar na ndege mpaka Arusha, mimi nilikuwa na show Babati jana. Arusha mpaka Babati ni masaa mawili au matatu. Kufika njiani kuna sehemu inaitwa Minjingo kama sikosei kuna wanyama wanyama hapo. Tulikuta pundamilia mmoja barabarani, alikuwa ameshavuka…sasa wakati gari pia haijavuka nae alikuwa anataka kurudi tena huko halafu gari ilikuwa speed kidogo, sasa katika kupigapiga break ndio gari ikapinduka.” Ameeleza Shetta.

“Gari imeumia sana lakini sisi hatukuumia hiivyo, ni maumivu tu ya kawaida. Hapa nilipo ndio naelekea hospitali kufanya checkup ya mwili kama kutakuwa na internal effects lakini kwa nje niko vizuri sana.” Ameongeza Shetta.

Ameeleza kuwa ilibidi show yake iahirishwe hadi jana jumamosi kwa kuwa kila mtu alikuwa amepata taarifa kuhusu ajali hiyo.

Katika hatua nyingine, rapper huyo ameeleza kuwa alikuwepo mtu aliyepokea pesa ya show hiyo kwa jina lake hivyo baada ya waandaaji kwenda Dar walifanikiwa kupata namba halisi ya Shetta ambaye walimuomba awasaidie kufanya show hiyo ili kulinda jina lao kuliko kuahirisha.

Hata hivyo, Shetta amesema tayari polisi wanamshikilia mtu aliyekuwa amewaunganisha waandaaji hao na Shetta feki na kwamba anatamani kuongea nae ili afahamu undani wa mchezo huo wa kitapeli.
 
Show anaenda kufanya babati,huku akitoka dar mpaka arusha kwa ndege,...siku hizi show zitakuwa zinalipa,Mana navyojua Babati ni kama kijijini tu sijui alijazaje ukumbi
 
Show anaenda kufanya babati,huku akitoka dar mpaka arusha kwa ndege,...siku hizi show zitakuwa zinalipa,Mana navyojua Babati ni kama kijijini tu sijui alijazaje ukumbi

labda hujafika babati siku za karibuni... babati ndio makao makuu ya mkoa wa manyara. pamekua saaannaaaa saaannaaaaa..ukiongezea na barabara ya lami direct from arusha, na pia singida.. na nyingne ya kwenda dodoma ipo under construction.. sio kijijini kama unavyodhani. nenda siku moja ukajionee. babati ni mji tena mkubwa tu na unagrow haraka sana.
 
Hebu niambie club mmoja ambayo msanii mkubwa anaweza kufanya show Babati,maana sijaona club pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…