Shibe inapoua mara 3 zaidi ya njaa - obesity kills more people than hunger

Bongo Pix Blog

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2011
Posts
213
Reaction score
33

Ni taarifa ya kusikitisha, kushangaza na kuudhunisha lakini ni kweli

Kwa katika kizazi hiki cha dotcom cha sayansi na teknologia, kizazi cha Ipad, smartphones ambapo karibia kila mtoto mpaka wa chekechea amenunuliwa, achilia mbali mabeki tatu, kizazi cha fesibuku, twita, wasap nk kizazi ambacho makampuni ya simu yanashindana kushusha ama kupandisha bando, lakini kwa bahati hakijui kabisa kutumia vifaa hivi muhimu kwa manufaa, bali kuchati masaa 24 pasipo kuongeza chochote kichwani, HII NI HATARI.

Kwamba sasa shibe ndio inachukua uhai wa watu wengi kuliko njaa, kuliko ajari, kuliko malaria, kuliko bunduki, hii inasikitisha sana, hii yote ni kwasababu ya mtindo wa maisha anaochagua kuishi, ndio ama wampeleka kaburini mapema ama anamaliza siku zake alizopangiwa na Muumba wake.

Lifestyles related diseases yalisababisha vifo zaidi ya milioni 36 mwaka 2008 kati vifo milioni 57 duniani, lakini mwaka 2012 vifo hivi viliongezeka na kufika milioni 38 kati ya vifo milion 56, yaani kwenye magonjwa mengine vifo vilipungua kwa milioni 1 lakini magonjwa ya mitindo ya maisha viliongezeka kwa milioni 2, makadirio ni kuwa vifo vitaongezeka maradufu ifikapo mwaka 2020, hizo takwimu ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani, ripoti zote 2 ziko online waweza kuzishusha na kudadavua kwa upole kabisa na ipad au smartphone yako, ukaisoma kwa muda wako,

Kwa wale MA GT na wanaomaanisha na wangependa kujua mengi zaidi BOFYA HAPA\

bali kwa wale wa midhaa midhaa, wa kuchat chat kupoteza muda hapo bila sababu, wasiojua dunia yaendaje ambao ndio wengi zaidi mitandaoni, hapa panakutosha, kuna kitu umepata.
Mungu awabariki sana.
 
Mazoezi ni muhimu kwa afya,si lazima kwenda gym,badala ya kuchat na kutazama TV muda wote,ni vryema ukatumia even1/2hr kwa mazoezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…