Binafsi naona tunaacha mchele mwingi na kutafuta mawe machache. context ya magale kurudi bungeni, inahusu hujuma na njama kali sana. kuna mtu alikufa, Magale aliwekwa ndani, akazuiwa kufanya kampeni na kuvumishwa kwamba katolewa kwenye ugombea ili kuwakatisha tamaa wapiga kura. kilicho muhimu ni kauli ya wapiga kura kwamba wamechambua mchele na pumba wakazitupilia mbali, pamoja na nguvu kubwa zilizotumika na dola. CHADEMA imeweza kudhihirisha kwamba inao uwezo wa kukusanya watu waliojipambanua kuwa ni wapambanaji kutoka kila kona. ni kweli mapandikizi wamo, na wenye tamaa zao wenyewe bado wapo. ndio maana CHADEMA bado inayo kazi ya kutorudia makosa ya ccm, na kuja na structure ya aina yake ambayo itahakikisha kwamba mafisadi na mandumila kuwili wanachujwa mapema, na chama kisonge mbele. tatizo sio kwamba magale anaweza kuwa ndumila kuwili. tatizo ni nini CHADEMA kitafanya katika mazingira hayo. CCM wameonesha njia isiyofaa. inashtaki watu kwa ufisadi, na kutamba kwa rekodi hiyo, na kisha inarudi kuwaombea kura jimboni kwao. huu ni uchafu na sioni kama ccm wameachana nao