gogo la shamba
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 6,669
- 2,165
Ndugu wanajamii katika kipindi cha TBC leo asubuhi,Shibuda na Serukambwa wanasisitiza kwamba,serikali mbili ndizo zinazotufaa kwa kuwa sisi ni wamoja hasa kwa jinsi mahusiano yetu yalivyoingiliana kuanzia kuoana,biashara NK.
Lakini mimi kama Gogo la Shamba nawashangaa sana kama wanayoyasema ni ya kweli kwa nini wasitake serikali moja?Kwa sababu wanazozisema wao ingestahili watake serikali moja,wanachoogopea kusema serikali moja ni kwa sababu wazanzibar hawaitaki serikali moja kwa kuwa hawataki serikali ya Zanzibar ipotee kuliko serikali ya Zanzibar ipotee wako tayari muungano ufe,sasa mimi nauliza kwa wale ambao pia hawapendi serikali ya Tanganyika ife unawapeleka wapi?
Mimi nionavyo hapo la msingi ni serikali tatu ili kila mmoja awe na serikali yake alafu kuwe na serikali ya ubia kati ya Tanganyika na Zanzibar au kama mapenzi yetu ni sawa basi zote tukubali serikali zetu zife tuwe na serikali moja ya muungano. Hebu wanajamii tuchangie hapo kwa kutoa sababu zinazokubalika tusifuate ushabiki.
Naomba kutoa hoja.