mimiamadiwenani
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 5,718
- 7,784
Kwema wakuu?
Nakumbuka kwa mara ya kwanza nilikuona kanisani, kwa Mchungaji Rasarasa mwenye mtoto ambaye kwa sasa anafanya kazi radio mawingu. Ulikuwa kijana mkimya, mpole na mnyenyekevu.
Nakumbuka kila asubuhi nilipofika ibadani, nilikukuta ukiwa umeshafika. Ulikuwa na nidhamu sana. Ulikuwa kijana mfano wa kuigwa pale kanisani.
Ulikuwa unaongoza kwa kuhamasisha mifungo pale kanisani, na kwenye makanisa jirani, uliyokuwa ukihudhuria kwa nyakati fulani fulani. Hukupoa!
Kumbuka ulivyokuwa una nguo moja tu, na hukuwa na nguo ya kubadili. Kumbuka yule mtoto wa Mchungaji Rasarasa alivyokuwa anakupa nguo zake uvae, chakula chake ule. Mkawa marafiki, akipigwa yeye umepigwa wewe, na ukipigwa wewe amepigwa yeye.
Kumbuka ulivyokuwa unatembea na vyeti kuomba ufadhili wa masomo. Kumbuka ulivyokuwa unalala kanisani, kumbuka brother.
Kipi kilikubadilisha? Kwa nini ukawa hivyo?
Kwa nini ukauza nafsi yako kwa shetani? Kwa nini ukaingia agano na shetani? Ulikosa nini???
Umebadilika mno brother.
Dah!
NB:
Hii ni hadithi tu.