Shida tunazozitoa mabroo tunaopenda Hip Hop

Shida tunazozitoa mabroo tunaopenda Hip Hop

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Mstari unaotenganisha Rap na uhuni ni mwembamba sana.

Mimi ni mmoja wa watu wanaopenda zaidi rap kuliko aina yeyote ya mziki. Ili roho yangu isuuzike kusikiliza mziki basi inabidi iwe rap. Zamani nikiwa dogo nilikuwa sipati shida kuupa moyo wangu kile unataka.

Sasa unakuwa bro, kinachosemwa rap ni uhuni inabidi ujitahidi kupunguza. Maana ukiweka rap hapa home na familia muda wowote Nas atatukana fu@#$ck police halafu ionekane dingi hapa hatuna.

Hakuna kitu kinakera kama upo ofisini umeamua kujiboost na ngoma kali za Jah Rule, halafu anakuja mtu anakuuliza bro kumbe na wewe huwa unasikiliza Hip Hop. Au anakuja mgeni hapo ofisini anakuta umeweka rap za Talib Kweli zinazungumzia harakati, halafu huyo mtu anakuangalia mara mbili mbili

Hata kupakia familia kwenye gari basi inabidi ujinyime unaweka zile nyimbo za Israel Mbonyi, ukishawashusha ndio unatia kitu cha Mitaa ya Kati-Imam Abas ft Kiroboto. Usipofanya hivyo utasikia "sasa baba yenu katuwekea mamiziki gani hayo" inabidi kumezea tu kujifanya hujasikia.

Tunaopenda Hip Hop tunabezwa sana, inaonekana tunasikiliza kitu cha hovyo
 
Mimi hata kuniuliza huwa hawawez mana lifestyle yangu tu ni hip hop tosha, nasikitika tu ikitokea tumeenda kunywa na washikaji huwa hawaniruhusu niunge Bluetooth na spika za kaunta.
 
Pole sana. Bora wewe, sisi wapenzi wa death metal ndiyo tunaonekana wadogo wa shetani au vichaa kabisa.
 
Bora Hip Hop...
Kuna mdingi aliwekaga singeli mpaka mkewe akamjia juu.
"Baba (fulani)! Na umri huu unatuwekea singeli kweli? Mbona hujiheshimu"
 
siku wakikuta una sikiliza watengwa si watahisi ume chizi!?
 
Playlist yangu mwaka huu ni Hip-hop tuu kwa sasa nimeanza na Dizasta vina ila soon nitazid kuongeza wasanii (Recommendation needed)

Nilud kwenye mada hapo nyuma nilikuwa nakuwa na ngoma 1500+ kwenye simu lakin nasikiliza 10 nyingine hasa kuunganisha Bluetooth nikaona kuwa na ngoma kwa ajili ya watu ni utumwa nimamua Kubaki na zile nasikiliza tuu watajua wenyewe hip-hop for everybody
 
Back
Top Bottom