Shida ya gari au lugha? Nisaidieni

Colea911

Member
Joined
Jul 20, 2014
Posts
24
Reaction score
5
Mambo,

Ningependa kuuliza maswali kuhusi misamiati ya kutengenza magari. Mimi ni msomaji wa kiswahili lakini nimeshindwa kuwaelezea mafundi shida zangu. Kwa mfano naomba usaidizi ya kutafsiri misemo hii kwa kiswahili:

"My car won't start"

"The battery does not have enough power/energy to start the car"

"I want to leave my car running for 5 minutes"

"the car is not charging the battery"

"lets push the car to jump start it"

"Should I start the car?"

Labda gari halitakuwa shida nyingi kama naweza kuwasiliana vizuri zaidi. Asanteni waungwana.

 
Aaah! Tupa kule. Mchina anakutengenezea gari yako inatoka bomba na lugha hajui. Hao mafundi vilaza tupa kule!
 
Mimi nafikiri kwa Lugha yetu ya Kiswahili Mafundi wengi/ watu wengi tunatumia Kiswanglish au labda niseme tunatohoa maneno ya kigeni kwenda Kiswahili.
Halistati badala ya Haliwaki.
Bateri haina nguvu ya kutosha kuwasha gari.
Ukweli mafundi wanachofanya ni kuacha injini izunguke kwa dakika tano.
Pia Gari haichaji bateri ila Altaneta ndio huchaji Bateri
Unaposukuma gari ili iwake (MANUAL TRANSMISION SYSTEAM) unachofanya ni kuzunguza ingini kwa kutumia matairi na giaboksi ili upate lile pigo la pili yaani kompresheni(mgandamizo) ili liwake.
Naweza kuwasha gari?

NB:Kuwaka .... Gari linawaka, Mashine inawaka, Injini inawaka, Jua linawaka, Taa inawaka, Tochi inawaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…