Shida ya Marefa wetu ni Umri, Elimu, Weledi au ushabiki??

Shida ya Marefa wetu ni Umri, Elimu, Weledi au ushabiki??

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Ukiondoa kiwango cha juu cha ushabiki wa mpira tulichonacho kuliko uhalisia wa timu tunazozishabikia, uduni wa wachezaji wetu, lakini pia Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu Tanzania inaharibiwa kwa asilimia sitini (60%) na uchezeshaji wa marefa wa mchezo huo.

Ligi yetu inaharibiwa sana na marefa wetu, na inaonekana hakuna timu ama"watu wa mpira" wanaoona Marefa wanaochezesha ligu Kuu ni tatizo. Inawezekana Timu na hao watu wa mpira wanafaidika na uchezeshaji mbovu wa marefa hao.

Tatizo ni nini? Umri walio nao, Elimu yao kuhusu mambo ya mpira, hawana mazoezi mengi hivyo hawana weledi au ushabiki kwa timu wanazozichezesha ndiyo unawafanya wachezeshe vibaya?
 
Gsm anawahonga sana
Kwa ivo na rushwa pia ni sababu!!??

Nasikia posho yao Marefa kwa mechi moja ni shilingi laki nne(400,000), sasa wahongaji wanajua kuchezesha vibaya adhabu yake ni kuzuiwa kuchezesha mechi tatu ambayo refa atakosa milioni moja na laki mbili (1,200,000). Wao wanampa kabisa hiyo hela, kisha ndiyo wanaongezea dau juu ya milioni moja na laki mbili.

Marefa kwa kujua kufungiwa si rahisi kiivyo, huchukua hiyo hela na kuchezesha vibaya na maisha yanaendelea. Othman Kazi alipojaribu kulisemea hili akafungiwa maisha kuwa Refa.
 
Mwamedi ndo anaongoza....the teh...
 
Na uduni wa timu hii ya tatu(referee's)ndio unachangia pia uduni wa ligi yetu
 
Lakini kwenye mechi nyingi tu hawa watu wanaboronga, sema mechi za Simba na Yanga ndizo watu mnazitolea macho. Lakini tuna marefa wenye viwango vya chini kabisa.

Nachelea kusema kwamba tuna marefa wa hovyo sana.
Unataka kuharibu mada yako nzuri kwa kukaribisha hoja za mashabiki maandazi humu ndani. GSM au Mo watahongaje mechi ya Kagera Sugar vs Ihefu? Kuna watu hawana vichwa vya kutosha kujadili mambo ya maana hivyo achana nao.
Ulichokileta hapa ni hoja nzuri sana na kwa muelewa atajua aliyeileta anatumia kichwa kutunza ubongo na siyo kifuniko cha shingo.
Kiujumla tatizo la marefa wa Tanzania cha kwanza ni uelewa. Uelewa wao kuhusu sheria uko chini kiasi cha kushindwa kutoa tafasiri halisi.
Mfano wa ubovu wa tafsiri ni tukio moja mechi ya Yanga mpira ulizunguka kipa akaushika nyuma ya mlingoti lakini ndani. Mwamuzi msaidizi akasema ni kona.inakuwaje kona?
Mwaka Jana nimeangalia mechi ya Mtibwa na Ruvu, mchezaji kampiga mwenzake teke walipoanguka chini kwa vile tu kamlalia. Refa kaona kawafuata maamuzi yake ya hekima ilikuwa kuwasuluhisha.
Tatizo la pili ni rushwa. Hili linahusisha mpaka viongozi wa mikoa. Mkuu wa mkoa husika anaunda timu ya kumkarimu refa ili timu ya mkoa wake ishinde. Hili bila ubishi Adam Malima na Umella pale MBEYA wanalijua vizuri.
 
Mkuu wa mkoa husika anaunda timu ya kumkarimu refa ili timu ya mkoa wake ishinde.
Kama Mkuu wa mkoa anashiriki unadhani nani tena anaweza kuzuia Marefa kuhongwa!! Vyama vya mipira vya mikoa navyo havishiriki?
 
Lakini kwenye mechi nyingi tu hawa watu wanaboronga, sema mechi za Simba na Yanga ndizo watu mnazitolea macho. Lakini tuna marefa wenye viwango vya chini kabisa.

Nachelea kusema kwamba tuna marefa wa hovyo sana.
Ni shida kubwa sana.
 
Back
Top Bottom