Habari viongozi na wadau wa TANESCO, hii shida narudia tena kuitandika hapa, njia hii ya umeme kutoka kimara baruti kwa miaka mingi haishi matatizo, toka enzi zile transfoma ipo juu hadi ikashushwa chini na mafundi wetu kidogo hali ikabadilika, likaja tatizo la umeme kupungua, ikawekwa transfoma nyingine pale darajani hali ikaimarika, sasa hivi tena shida imerudi tena, tena kubwa, ikifika saa 1 usiku umeme ni afadhali ya kibatari, kuunguza vitu ndio kila kukicha, tunaomba mtusaidie maana hali sio nzuri, umeme unasaidia vitu vingi, ikiwemo watoto kusoma n.k.
Nashauri jioni timu ya emergency ipite muda huo wa saa 1 hadi saa 4 wajionee taa zinamulika afadhali ya vibatari.
Asanteni
Naomba kuwasilisha
Nashauri jioni timu ya emergency ipite muda huo wa saa 1 hadi saa 4 wajionee taa zinamulika afadhali ya vibatari.
Asanteni
Naomba kuwasilisha