A
Anonymous
Guest
Habari wanafamilia wa JF,
Niende moja kwa moja kwenye hoja:
Kumekuwa na shida ya makusudi ya upatikani wa Maji katika eneo la Ubungo Kibangu na maeneo jirani kama Riverside.
Hapo awali maji yalikuwa yakitoka Kwa wiki mara mbili, baadaye ikawa yanatoka siku moja kwa wiki kati ya Ijumaa hadi Jumapili,lakini hivi karibuni maji hayatoki kabisa hadi mwezi mzima, wananchi wa eneo hili wanapata tabu sana, dumu moja la maji ya chumvi ni shilingi 300-500 na maji yasiyo na chumvi ni 1,000-1,500 kwa dumu.
Imekuwa kero kubwa sana, lakini magari ya kuuza Maji yanapishana na inasemekana ni ya kigogo mmoja anayefanya kazi DAWASA na ndiye anayehakikisha maji hayapatikani eneo hili ili afanye biashara.
Kupitia jukwaa hili tunaomba taarifa hii iwafikie wahusika na hasa Waziri wa maji Aweso aweze kuchunguza jambo hili.