BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Erick Shigongo ameshauri Serikali kuanzisha Mfuko wa Taifa wa Ubunifu ambao utasaidia watu kufanya utafiti na kuzalisha bidhaa.
Shigongo ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 15, 2022 wakati akiwasilisha mada yake ya ubunifu na ujasirimali katika Kongamano la tatu la maendeleo ya biashara liloandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).
Shigongo ambaye ni mbunge wa Buchosa (CCM) amesema Taifa lolote ambalo haliwekezi katika ubunifu haliwezi kukua.
Amesema Tanzania ina wabunifu wengi ambao wanaweza kuibadilisha nchi ikawa kituo (hub) cha teknolojia barani Afrika.
“Lakini pengine wanakutana na changamoto kwenye maisha yao. Kama tumedhamiria kwenda mbele ni lazima kuwekeza katika ubunifu,”amesema.
Shigongo amesema wapo vijana wengi wabunifu lakini wanashindwa kusogea mbele kwasababu mitaji yao ni midogo hivyo uvumbuzi wao wameuweka ndani.
“Wameshindwa kubadilisha uvumbuzi wao kuwa biashara kwasababu ya ukosefu wa mitaji. Kama tunataka kuongeza pato la Taifa, pato la Mtanzania na ili uchumi ukue lazima kuweza teknolojia na ubunifu. Ni lazima tuweke fedha kwa ajili ya ubunifu,” amesema Shigongo.
Alitoa mfano wa nchi ya China ambayo kwa muda wa miaka 10 haikuwa na bilionea hata mmoja lakini waliamua kuwekeza katika jambo hilo leo nusu ya mabilionia ni Wachina na kwamba Tanzania inaweza kufanya hivyo.
Amesema hilo litawezekana kwa kuanzisha Mfuko Taifa wa Ubunifu ambao utawezesha wabunifu kufanya utafiti utakaovumbua na kutengeneza bidhaa zitakazoingia katika soko.
Amesema hilo limefanywa na nchi nyingi ikiwemo Afrika Kusini na Kenya ambapo watu wao wamewezeshwa na mifuko yao kufanya ubunifu na kuingiza biashara sokoni.
Akimwakilisha Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Mussa amesema bado kumekuwa na msukumo mdogo wa kufanya tatifi na kusambaza matokeo na hata kuyatumia.
“Bado katika nchi zetu tumejenga tutamaduni kufanya tafiti ni jukumu la wataalam wanaokaribia kustaafu pamoja na wale wanaofanya degree (shahada za uzamivu), lazima tuwe na mikakati ya pamoja ya kutayarisha watafiti tangu ngazi ya awali,” amesema.
MWANANCHI