The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, ametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 10 kusaidia kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Majengo, Kata ya Ilenza, ambayo ujenzi wake ulikwama kwa takriban miaka 15.
Akiwa kijijini hapo Machi 07, 2025 Shigongo amewahimiza wakazi wa Kijiji cha Majengo na Buchosa kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, akisisitiza kuwa ushirikiano wa jamii ni muhimu kwa mafanikio ya miradi mbalimbali.
Pia soma: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Ameeleza kuwa ni muhimu kwa jamii kushirikiana katika kuanzisha miradi ili serikali iweze kusaidia kukamilisha na kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa wakati bila kuingiza siasa kwenye mambo ya msingi kama afya za watu