Pre GE2025 Shigongo atoa milioni 10 kukamilisha ujenzi wa Zahanati uliosimama kwa miaka 15 Buchosa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, ametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 10 kusaidia kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Majengo, Kata ya Ilenza, ambayo ujenzi wake ulikwama kwa takriban miaka 15.

Akiwa kijijini hapo Machi 07, 2025 Shigongo amewahimiza wakazi wa Kijiji cha Majengo na Buchosa kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, akisisitiza kuwa ushirikiano wa jamii ni muhimu kwa mafanikio ya miradi mbalimbali.

Pia soma: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Ameeleza kuwa ni muhimu kwa jamii kushirikiana katika kuanzisha miradi ili serikali iweze kusaidia kukamilisha na kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa wakati bila kuingiza siasa kwenye mambo ya msingi kama afya za watu
Your browser is not able to display this video.
 
Mama kawezesha zahanati kila Kijiji, huyu anatuambia Nini?
 
Huyu jamaa hovyo sana. Alikuwa USA sijui kanisani anahamashisha wazungu waombe eti Trump abadili mawazo arudishe misaada aliyoondoa kwa nchi maskini. Ukichunguza utakuta alisafiri kwa business class kwena na kurudi. Uchaguzi unakuja hivyo wengi watajifanya kukumbuka wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…