SHIKAMOOO Natoa Kwa WALE WAKUBWA ZANGU.

SHIKAMOOO Natoa Kwa WALE WAKUBWA ZANGU.

Ibrahim Mussa

Member
Joined
Jan 4, 2013
Posts
6
Reaction score
1
Shikamoni mliomo humu ndani kaka & dada zangu. Kwa kweli nimefarijika mdogo wenu kwa KUIJUWA mtandao huu ambao watu wanajadiliana mambo mbalimbali kama elimu, afya,vichekesho, siasa n.k

Jina langu naitwa Ibrahim Mussa kama nilivyopewa na wazazi wangu, nina umri wa miaka 16. Ni mwanafunzi wa darasa la saba na mwaka huu nategemea kuingia form One. Ninapenda kuingia kwenye Internet na kuangalia vitu mbalimbali ndo siku 1 nilipokuwa nasearch www.google.com nikabahatika kukutana na mtandao huu wa Jamiiforums.
Kwa hapa kijijini nilipo najihisi kama ni mwenye bahati kuujuwa mtandao kama huu mana kuna vijana wengine wao akiingia kwenye internet ni kudownload chonda kwenda mbele hata kuingia mitandao ya kusoma habari muda huo hawana.
Kwa kweli ninafuraha sana kwa hili.
NAOMBA MUNIKARIBISHE WAKUBWA ZANGU AHSANTENI.
 
Karibu, nikuambie kitu? Hapa wengi wetu tunatumia ID na si majina yetu halisi ila kama kwako huoni tatizo sawa tu.
 
'''''marhaba, na karibu......'''''
 
Ahsante, mimi nimeona nitumie jina langu labda humu kuna watu watakuwa wananifahamu !!
 
Marhaba kijana.....Karibu sana JF, jisikie upo nyumbani
 
Nani kakwambia wadogo hawatoagi zawadi! Sasa mbona uko mikono mitupu au ndo umeshamaliza zawadi zote? Karibu sana, mimi pia sio mwenyeji sana ila utawakuta wenyewe watakujulisha kona zote za jumba hili. Ukitaka tuonane uwe unakuja basi kwenye kijiwe cha mabisiness na wajasiliamali tubadilishane mawazo.
 
Back
Top Bottom