Shilatu awafariji waliopata maafa Mihambwe

Shilatu awafariji waliopata maafa Mihambwe

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Na Mwandishi wetu Mihambwe,

Mwenyekiti Kamati ya ulinzi na usalama Tarafa ya Mihambwe ambaye pia ni Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu mapema leo Februari 22, 2022 amewafariji wakazi wa vijiji vya Mihambwe na Ruvuma kufuatia jana Jumatatu Februari 21, 2022 kutokea kadhia ya upepo mkali uliombatana na mvua kubwa ulioezuea paa za nyumba 15, Madarasa 8, ofisi 3 na nyumba 2 za Waalimu. Shule zilizopatwa na kadhia hiyo ni shule ya msingi Mihambwe na shule ya msingi Ruvuma ambazo zipo vijiji vya Mihambwe na Ruvuma.

"Kwanza nawapa pole kwa Wananchi, Waalimu na Wanafunzi wote waliopatwa na majanga ambayo yalijeruhi Mtu mmoja na hakuna kifo.

Nikiwa kiongozi wenu wa Tarafa nimeguswa na kuamua kufanya ziara hii fupi kujionea hali halisi, kuwapa pole na kuwafariji. Serikali ipo pamoja nanyi bega kwa bega kuhakikisha Watoto wetu wanaendelea kusoma kama awali, miundombinu ya Madarasa inarejeshwa vyema haraka iwezekanavyo kama ilivyokuwa awali na Wananchi wanaendelea na maisha yao kama kawaida". Alisema Gavana Shilatu

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na uongozi wa vijiji na shule kutembelea makazi na Madarasa yaliyopata uharibifu mkubwa ambapo aliongea na Viongozi, Wananchi, Waalimu na Wanafunzi ambao wameonyesha utulivu mkubwa na ushirikiano nyakati zote.

FB_IMG_1645547603401.jpeg
FB_IMG_1645547620549.jpeg
FB_IMG_1645547634359.jpeg
FB_IMG_1645547638159.jpeg
FB_IMG_1645547642470.jpeg
 
hakuna hiko cheo cha mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Tarafa
Embu acheni kuhadaha raia shenzi kabisa nyie
 
Gavana Shilatu hongera sana ndugu yangu, Kazi iendeleee popote.
 
Back
Top Bottom