Membe S K
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 1,389
- 1,253
Mkuu kwanini tusisome wote ili tuweze kuelewa hiyo lugha wote? inabidi tuwafuate huko huko waliko ndio watashindwa kutuongopea.
Mkuu masomo yapo ya aina nyingi, wapo waliosomea uganga na wana uelewa mdogo wa saikolojia, kadhalika mtu moja hawezi kuwa amesoma masomo yote duniani. Unachokijuwa wewe kwa undani sio nachokijuwa mimi, na usomi wako hautaleta faida kwangu kama utashindwa kunieleza kile unachokijuwa kwa urahisi na kwa lugha nayoijuwa mimi; hapo elimu yako itakuwa imeshindwa kutoa faida husika.
Mkuu kuna mtu mmoja ametoa excuse ya kijinga sana, anasema kuporomoka kwa uchumi wa Tanzania kunatoka na mtikisiko wa uchumi na fedha, na akasema kama mambo yangekuwa kawaida basi hali ya uchumi wa Mkapa ingeendelea mpaka sasa. Lakini akasahu kuwa Kenya Rwanda na Uganda nazo pia zilielewa kwenye mtumbwi huo huo na uchumi wao hujaporomoka ki vile. Kwa hiyo "ceteris persibus" haikuwepo Tanzania tu ila kwa jirani zetu ilikuwepo.
Mkuu angalia husichanganye HYPOTHESIS na THEORY. Huyo aliyesema uchumi wa Tz umezamishwa na tikisiko la uchumi wa dunia ametoa hypothesis tu wala sio theory, na ceteris paribus inalinda theory sio hypothesis.