Shillingi mil 600+, VPL nayo tutapindua meza

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Mabingwa mara 27 Tz na mabingwa mara 3 mfulilizo,Yanga leo imeweza kufuzu katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho,japokuwa tumefungwa 1-0, lakini ushindi wa nyumba wa goli 2-0 umekuwa na faida baada ya maana agregate 2-1.Ndani ya miaka miwili Yanga imeweza kufuzu kwa hatua hiyo baada ya mwaka 2016 kufikia hatua hiyo baada ya kuitoa timu ya Sagrada ya Angola kwa matokeo kama haya.Makundi yatapangwa tarehe 21-04-2018,huku Yanga ikiweka kibindoni dola laki 3,sawa na zaidi ya shilling mil 600.

Japo msimu huu Yanga imekuwa na vikwazo vingi ikiwemo wachezaji wengi kuwa majeruhi,ukosefu wa fedha hasa baada ya mfadhili wetu Manji kujiweka pembeni,hali iliyopelekea kutokuwa na matokeo mazuri hata katika ligi ya mabingwa Africa na ligi kuu VPL.Nawapongeza viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi bila kuwasahau mashabi na wanachama,kwa umoja na mshikamano hadi kufikia hatua hii ya leo.Msimu huu hata tukikosa ubingwa kufuzu hatua hii itatufuta machozi wan yanga.

Ipo siku kila mtu ataishabikia Yanga,niwaambie tu Simba kuwa karibuni sana pale kwa mchina kuwashabikia wapinzani wetu maana nyie ndo kazi yenu,wenzenu ndo tunasonga ivyo,nyie endeleeni kupiga mziki wa taarabu na MC wenu Hajji Manara,mtajikuta hata VPL linatua Jangwani.

DAIMA MBELE,NYUMA MWIKO
 
Pole sana haya kalipe madeni
 
we jamaa huelew maana ya ushabiki...sasa unataka kila mtu ashabikie yanga na hapo mpira si ndo utakua umeisha bongo au...mana itakua haina maana.....punguza kumpwaya
 
Mashabiki wa Mikia fc wamejificha uvunguni. Wamenuna hatareee. Heboooo nani kakwambia Yanga ni wa mchezo mchezo....
 
Haya mambo ya ushabiki ndio yalishanishinda kitambo. Ni zaidi ya upinzani wa kisiasa. Nongwa mwanzo mwisho. Lakini mchezaji wa timu moja anaweza kuhamia timu pinzani wakati wowote kwa maslahi yao binafsi.

Sasa kama kocha au mchezaji anahamia kwa mahasimu, kwanini washabiki kuvutana mashati na kuweka uhasama wa kupitiliza? Ushabiki uwe kistaarab.
 
Hongera wa Yanga kwa kuingia makundi kombe la shirikisho.
Ila msishangilie sana msijifanye tumesahau kua nyie mlikua mnashiriki klabu bingwa Afrika ndo ilikua lengo lenu.
Nilichokiona kingine wana Yanga wengi pamoja na viongozi wao wanashangilia kupata 600. Kitu ambacho kinaonesha kua hawana malengo yoyote kwenye mashindano. Tusubiri vipigo kwenye hatua za makundi .
Mana lengo la CAF kutoa 600 sio kwamba ni bingwa ila ni kuisaidia Timu kujiandaa kwenye mashindano.
 
Back
Top Bottom