Shilole kushoot video yake na Justin campos South Afrika

Kidingi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2012
Posts
1,872
Reaction score
1,832
Shilole anatarajia kusafiri kwenye nchini Afrika Kusini kufanya video ya wimbo wake Nyan'ganyan'ga na Justin Campos. Shishi ameiambia Bongo5 kuwa wiki ijayo atasafiri kwaajili ya kwenda kufanya kazi hiyo.

Nashukuru Mungu ngoma yangu (Nyan'ganyan'ga) inafanya vizuri katika media mbalimbali. Hapa ninavyoongea nipo kwenye maandalizi ya kwenda kufanya video Afrika Kusini. Video nafanya na Justin Campos na maandalizi yapo tayari wiki ijayo nitasafiri, amesema Shilole.

Hata hivyo Shilole hakuweka wazi iwapo kazi hiyo itatoka mwaka huu au mapema mwakani.

SOURCE ; BONGO5

Popote ilipo management yake, naipongeza saana. Wasanii wengi wamejitutumua kuwekeza kwenye video kali, nimefurahi na shilole ni mmojawapo ambae nae ataanza kuonekana kwenye vituo vikubwa vya tv Afrika mikiwemo MTV BASE, na TRACE INTL.. Hapa baadhi ya wasanii waige nao wajifunze kuwekeza video kali wakiwemo jamaa hawa Rich mavoko na Barnaba boy..
 
shilole ni msanii mkubwa sana,anajua kuimba kuliko msanii yeyote bongo,kiukweli anajua sema wenye roho mbaya ndo wanambania.
 
Akumbuke tuu kuvaa kiheshima asjie vunja maadili huko kwa mandela
 
shilole ni msanii mkubwa sana,anajua kuimba kuliko msanii yeyote bongo,kiukweli anajua sema wenye roho mbaya ndo wanambania.

kweli mkuu, itabidi diamond aombe collable moja hapa
 
Shilole anazidi kuwa tishio. Huyu dada kinachombeba ni hii kutulia na mpenzi mmoja (Nuh Mziwanda) hivyo kujiepusha na stress za mapenzi. Akiendelea hivi atamtimulia vumbi Diamond kabla hata ya Machi 2016.
 
Safi sana shishi baby kwa kuona mbali na inaonyesha pesa unazo ( maana kufanya kazi nje ya bongo haswa S.A si pesa ya kitoto)
 
kweli mkuu, itabidi diamond aombe collable moja hapa
asante,asiyekubali vokali za shilole hajui mziki,sitashangaa kina shakashaka,mbilia bel,yondo sister kuja kuomba msaada wa shilole kwa kolabo ili warudi kwenye chati
 
Big up Shilole.yaani kukosa wewe mziki wa Tanzania ungepotea kwenye ramani. Afrika nzima inasubiri kwa hamu hicho kichupa.
 
Hivi kun mtu mwenye masikio mazuri kabisa yanayofanya kazi na kuchuja sauti vizuri anayeweza kumuita shilole mwanamuziki?mshamwonaga akiimba live alivyo chenga?
 
Hivi kun mtu mwenye masikio mazuri kabisa yanayofanya kazi na kuchuja sauti vizuri anayeweza kumuita shilole mwanamuziki?mshamwonaga akiimba live alivyo chenga?

Shilole ana uwezo mkubwa wa kuimba live kuliko mwanamuziki yoyote wa kike kwa Afrika mashariki kwa sasa. Waulize wadau wa Marekani na Ubegiji kwanini anapewa shoo nyingi za huko kwa dau lolote lile. Alipiga shoo masaa 3 nonstop anacheza na kuimba. Akirudi South Africa ataanza kuimba na live band
 
Teh teh yaani comments za hii post nimejikuta nacheka pekeangu kwa sauti

Yote kwa yote hongera shishi baby
 
nasikia juzi kati Jenifa ropez alimuomba collabo shilole akachomoa.! kwakweli tunajivunia msanii wetu
Shilole hakuchomoa ni kwamba Jlo alitoroka studio kwa kuhofia kufunikwa. Hiyo ilikuwa ni wakati Shishy alipofanya music tour kwenye majimbo ya Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…