Shilole: Nitagombea Ubunge Igunga

Shilole: Nitagombea Ubunge Igunga

Deshmo

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
4,819
Reaction score
4,263
Shilole bado ana nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Igunga, lakini anahofia kuwa maisha yake yanaweza kuwa hatarini!

Shilole ameiambia Bongo5 kuwa amepokea simu nyingi kutoka Igunga zinazomtaka ajitose kuwania nafasi hiyo, lakini bado yupo njia panda.

"Unajua siasa ni ngumu mimi bado nipo kwenye mjadala wa kugombea na hii ni baada ya kuona watu wanataka kuongozwa, lakini bado nafikiria,"amesema. "Nikiwa tayari nitagombea kupitia CCM.

Kitu ambacho kinaniogopesha kiukweli ukiangaliwa watu waliopita ni vijana tu wanakufa mapema kutokana na mambo ya siasa. Siasa
inahitaji moyo sana mimi ni muoga sana,naogopa kufa watu wanauwana! Mtu unatamani lakini ndo hivyo," ameongeza.

"Mimi napigiwa simu nyumbani Igunga, watu wengi sana kila mmoja ananiambia ‘tunakuhitaji ugombe yaani baada ya Rostam wananihitaji mimi! Mimi bado nipo njia panda mpaka sasa hivi lakini muda ukifika kila kitu mtasikia."

Chanzo: bongo5
 
mmmh CV gani aliyonayo mpaka wananch wamuombe awaongoze
 
"Baada ya Rostam wananihitaji mimi"

Kumbe Rostam bado ni mbunge wa Igunga!!
 
viroba + gongo +wanzuki + mtindi + cha arusha + njaa + mziwanda + ugali = jokes at work
 
Chadema wameufanya ubunge kuwa kitu rahisi,sugu katuharibia bunge.
 
Back
Top Bottom