Shimo hatarishi barabara ya Uhuru , Kariakoo

Mulama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
3,036
Reaction score
1,808
Barabara ya Uhuru kwenye makutano ya mtaa wa Likoma eneo la Kariakoo pembeni ya Benki ya Akiba kuna shimo kubwa lililoachwa na wajenzi wa Barabara ambapo ni zaidi ya mwaka sasa.

Shimo hili ni hatarishi sana kwakuwa hata wauza nguo za kushikilia mikononi wanalizunguka shimo hilo muda wote ikiwa ni pamoja na wapita njia kuelekea madukani.

Yawezekana Serikali yetu inayojari sana watu wake inangojea kutuma salamu za pole kwanza ndipo lizibwe!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…