Shimo la choo kujaa maji

Shimo la choo kujaa maji

trigeminal

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2015
Posts
1,944
Reaction score
2,283
Nilichimba shimo la choo kipindi cha kiangazi lilikua fresh tu na likafunikwa juu, tatizo imeanza kipindi cha masika maji yanatokea chini na shimo linajaa maji.

Wataalam tusaidiane hapo nitumie njia gani?

NB: Chini halijapigwa zege limejengewa pembeni tu kwa mawe
 
water table iko juu, ila pamoja na waterproofing (check reliable materials at NABAKI AFRIKA) pia inabidi ulijenge litokeze juu zaidi ya usawa wa paving blocks
 
Pole sana kwa tatizo hilo ardhi yako ina maji kuna njia mbili za kukimbia hilo tatizo ya kwanza uingie gharama kujenga mashimo mawili moja tayali umejenga shimo la kwanza septic tank lazima lisakafiwe kwa ndani lisi ruhusu maji kuingia tafuta fundi ujenzi anayejua akuelekeze ujenzi wake hili kazi yake ni kupokea kukimengenya kinyesi kupitia bakteria anarobic na arobic then kupelekea maji kuja juu na kuingia kwenye shimo hilo la duala ambalo una lalamika kujaa maji hapo utakuwa umedhibiti kutojaa kwa shimo lako la choo...

Njia ya pili japo si ya uhakika sana ni kutenganisha mifumo ya maji taka soil na waste..Waste ni maji ya bath jikoni yape mfumo wake na soil ni mkojo na kinyesi yape mfumo wake so (Two system) hii itasaidia kwa kiasi flani...

Kumbuka kuwa
Shimo la choo likiwa na maji basi kinyesi ni ngumu kumengenywa so kinyesi kinabaki kilivyo na choo kinajaaa haraka plus na maji

Pili chemical kama jiki na baadhi ya sabuni shampool zina ua bakteria wanao kula na kumengenya kinyesi so ina pelekea kufa..

Ni vizuri maji ya jikoni bafuni na basin kutenganishwa kulinda hawa bakteria na shimo lisijae haraka
 
Liache ivo ivo. Maji ya shimo hujaa na kupungua kulingana na water table. Kwa matumizi ya kawaida, halitojaa hadi kufurika.
changamoto ni kipindi cha mvua inajaa mpaka juu kabisa hadi nimeshindwa kuhamia maana msimu huu limejaa top nasubiri mvua ziishe
 
Pole sana kwa tatizo hilo ardhi yako ina maji kuna njia mbili za kukimbia hilo tatizo ya kwanza uingie gharama kujenga mashimo mawili moja tayali umejenga shimo la kwanza septic tank lazima lisakafiwe kwa ndani lisi ruhusu maji kuingia tafuta fundi ujenzi anayejua akuelekeze ujenzi wake hili kazi yake ni kupokea kukimengenya kinyesi kupitia bakteria anarobic na arobic then kupelekea maji kuja juu na kuingia kwenye shimo hilo la duala ambalo una lalamika kujaa maji hapo utakuwa umedhibiti kutojaa kwa shimo lako la choo...

Njia ya pili japo si ya uhakika sana ni kutenganisha mifumo ya maji taka soil na waste..Waste ni maji ya bath jikoni yape mfumo wake na soil ni mkojo na kinyesi yape mfumo wake so (Two system) hii itasaidia kwa kiasi flani...

Kumbuka kuwa
Shimo la choo likiwa na maji basi kinyesi ni ngumu kumengenywa so kinyesi kinabaki kilivyo na choo kinajaaa haraka plus na maji

Pili chemical kama jiki na baadhi ya sabuni shampool zina ua bakteria wanao kula na kumengenya kinyesi so ina pelekea kufa..

Ni vizuri maji ya jikoni bafuni na basin kutenganishwa kulinda hawa bakteria na shimo lisijae haraka
Hii njia naona kama inafaa lakini ni ngumu Kwa sababu humo humo chooni ndo bafuni tunakunya humo tunakoga na sabuni humo na kukojowa Hadi kufua humo, Sasa kutenganisha ili maji yatakayolinda wale wadudu wanaochakata kinyesi utatenganisha vipi? Ama labda uelewa wangu mdogo.
 
Nadhani hiyo ni kwa wale wamejenga bafu tofauti na choo au choo cha kukaa na bafu humo humo hapo ni rahisi kutenganisha maji taka
 
Kwa haraka eneo lako lina sifa mojawapo ya ntakazotaja ama zote...
A.Water Table ipo juu.
-Mwamba mgumu wa kuzuia maji upo karibu na ardhi.
B.Altitude ipo chini.
-Kina kutoka usawa wa bahari kipo chini ya mita 1.

So ,eneo lako Halifai kwa mfumo wa choo wa kupotezea maji ardhini (Soakway pit).
-Hapo hakuna habari za kutenganisha sijui mfumo wa vyoo.
-Usidanganyike na habari ya mashimo kutojaa kwa mda mrefu

Kwa eneo lako,mfumo wa Mashimo mzuri ni wa kuhifadhi maji na kuchukuliwa na magari ya maji taka.
 
hii ishu imenikuta hata mimi, yani mvua ikipiga sana lazima lijae mpk juu....... likipiga jua yanaanza kupungua......

ila kuna mtu kaniambia ninaweza kujenga mtaro mkubwa, napanga mawe then juu natoboa shimo ili kufanya maji yaje kwenye mtaro, then juu nafunika na karatasi nylon afu ndii nafukia.......

hii itasaidiamaji yakifika level flan yasiendelee kupanda yanakua yanaingia kwenye mtaro (huu mtaro upana unakua 1m na urefu walau mita 4-5, kimo ft 4)
 
Huo mfumo,hauna tofauti na choo cha shimo...Kama ardhi yako ina Tabia hiyo ya kujaa maji,huo mfumo hautosaidia kitu...
Hayo mawe huwa kwa ajili ya kuzuia mchanga usijae kwenye hiyo trench...
According to data ulizotoa, either uweke mfumo wa

choo kupeleka majitaka kwenye chambers za jiji.
au
mfumo wa kuhifadhi maji,na kuja kuchukuliwa na gari za maji taka.  
 
Nilichimba shimo la choo kipindi cha kiangazi lilikua fresh tu na likafunikwa juu, tatizo imeanza kipindi cha masika maji yanatokea chini na shimo linajaa maji.

Wataalam tusaidiane hapo nitumie njia gani?

NB: Chini halijapigwa zege limejengewa pembeni tu kwa mawe
Nishawahi kupost hii inshu..pitia post zangu ila kwa kifupi tu ndugu

Usiingie gharama kubwaaaaa,fanya hivi

Bomba linalotoa maji ndani kupeleka kwenye shimo usilichimbie chini...lifanye limwage maji kwa juu ya shimo..yani kama vile maji ya bomba la mvua bafuni yanavyomwagika,sasa bomba lako limwage maji kwa juu

Hapo hata mvua inyeshe vipi kaka shimo halitajaa(nimefanya hv kwangu na water table ipo juu sana) na tatizo likakata

Hujiulizi kwa nn vile visima vya zamani vya kuchimba hta mvua inyeshe vipi havijai maji mpk juu yakapitiliza na kumwagika?

It's nature...
 
Ulitakiwa kulisakafia kabisa pembeni na cement kali na ile waterproof cement ila chini uweke tu zege
sawa ntafanya hivo kiangazi kwakua bado sijaanza kulitumia
Kama utazingatia ushauri huu sakafia na chini kote kusiwe na njia yoyote inayoruhusu maji kupita kusakafia kwenye kingo hakuyazuii maji kuingia yatapanda kutoka chini na still litajaa.

Kama lina urefu kuzidi 12 ft acha usifanye chochote mvua ikikata maji yataondoka yenyewe but kama urefu ni pungufu ya hapo sakafia lote tu japo hii nayo itakupa gharama za kunyonya maji machafu mapema kwa sababu utakuwa umelinyima uwezo wa maji kuondoka kwenye udongo wakati wa kiangazi.
 
hii ishu imenikuta hata mimi, yani mvua ikipiga sana lazima lijae mpk juu....... likipiga jua yanaanza kupungua......

ila kuna mtu kaniambia ninaweza kujenga mtaro mkubwa, napanga mawe then juu natoboa shimo ili kufanya maji yaje kwenye mtaro, then juu nafunika na karatasi nylon afu ndii nafukia.......

hii itasaidiamaji yakifika level flan yasiendelee kupanda yanakua yanaingia kwenye mtaro (huu mtaro upana unakua 1m na urefu walau mita 4-5, kimo ft 4)
Huo mtaro unauelekezea wapi?
 
Nishawahi kupost hii inshu..pitia post zangu ila kwa kifupi tu ndugu

Usiingie gharama kubwaaaaa,fanya hivi

Bomba linalotoa maji ndani kupeleka kwenye shimo usilichimbie chini...lifanye limwage maji kwa juu ya shimo..yani kama vile maji ya bomba la mvua bafuni yanavyomwagika,sasa bomba lako limwage maji kwa juu

Hapo hata mvua inyeshe vipi kaka shimo halitajaa(nimefanya hv kwangu na water table ipo juu sana) na tatizo likakata

Hujiulizi kwa nn vile visima vya zamani vya kuchimba hta mvua inyeshe vipi havijai maji mpk juu yakapitiliza na kumwagika?

It's nature...
Hapa sijakuelewa kabisa

"Bomba linalotoa maji ndani kupeleka kwenye shimo usilichimbie chini...lifanye limwage maji kwa juu ya shimo..yani kama vile maji ya bomba la mvua bafuni yanavyomwagika,sasa bomba lako limwage maji kwa juu"

Bomba gani linalotoa maji ndani?
 
Back
Top Bottom