SoC01 Shina moja la Mahindi hulipwa Tsh 60/= mifugo inapokula mazao fidia inayowatesa wakulima

SoC01 Shina moja la Mahindi hulipwa Tsh 60/= mifugo inapokula mazao fidia inayowatesa wakulima

Stories of Change - 2021 Competition

ROJA MIRO

Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
52
Reaction score
56
Ripoti ya wizara ya mifugo kwa mwaka 2019 inaonesha kwamba sekta ya mifugo inachangia 6.9% ya pato la taifa,na kwa upande wa taarifa ya wizara ya Kilimo ya mwaka 2020 inaonesha kwamba sekta ya Kilimo inatoa robo tatu ya mauzo ya nje ya bidhaa,inachangia 95% ya mahitaji ya chakula nchini,26.8% ya pato la taifa,30.9% ya fedha za kigeni na inatoa ajira kwa zaidi ya 75%.

Hapa nilitaka kuonesha uhusiano wa sekta hizi mbili za mifugo na kilimo katika uchumi wa Taifa na kwa takwimu hizo nadhani tumeona namna ambavyo sekta hizi zinavyoweza kuwa msaada mkuwa kwa watanzania kujiajiri wenyewe kupitia kulima na kufuga.

Pamoja na umuhimu wa sekta hizi bado kuna chamoto kadhaa zinazojitokeza na wakati mwengine kuibua ugomvi na tumekuwa tukishuhudia migogoro ya wafugaji na wakulima nchini kote,ila kama hiyo haitoshi pale mifugo inapokula mazao ya mkulima fidia inayolipwa wakulima wameitaja kwamba ni ndogo ukilinganisha na gharama ambazo wamekuwa wakizitumia kuandaa mashamba yao.

Sasa hapa tusiwe na shahidi marehemu kama wanavyosemaga wajuzi wa misemo,namaanisha naenda kwa mifano hai kutokana na data na takwimu sahihi,kwa mfano tu waraka wa fidia kwa mkulima pale mazao yanapoharibiwa na mifugo wa mwaka 2011 umetoa bei za fidia na hapa nitatolea mfano wa mazao mawili ili nisimchoshe sana msomaji .



Fidia.

Kwa mfano kwa zao la mahindi kama ng’ombe akila mahindi shina moja litalipwa jumla ya shilingi 60, na endapo mifugo ikiharibu mnazi basi fidia hiyo inatathimini kwamba mnazi huo utavunwa nazi 100 kwa kipindi cha mwaka mmoja na nazi moja italipwa shilingi 500 hivyo kwa mnazi mkulima atalipwa shilingi 50,000.


Gharama za Kilimo.
Kwa nchini Tanzania wakulima nimewagawanya katika makundi mawili,wanaotumia jembe la mkono na wanaotumia Trekta ambapo pia gharama hutofautiana kulingana na vitendea kazi ama pembejeo ambazo zimekuwa zikitumiwa na wakulima.Miongoni mwa wakulima wanaotumia jembe la mkono wanasema kwamba kumkodi mtu akulimie kwa Heka 1 ni sawa na Elfu 60,na kupalia shamba ni sawa na elfu 50 na wataalamu wanshauri mkulima apalie si chini mara 2 ndani ya msimu husika hivyo kulima na kupalia kwa heka 1 ni sawa na Tsh 160,000/=

Endapo kila mita 1 unapanda mbegu mbili na heka 1 ina ukubwa mita 70 upana na urefu maana yake ni sawa na 70 mara 70 mara 2.



NB:
Ufafanuzi (70 ni mita za shamba pande zote na 2 nI idaadi ya mbegu unazoweka kwenye kila shimo hivyo kwa ujumla shamba hilo la Heka 1 litakuwa na mashina 9800 mara Tsh 60 itakuwa sawa na 588,000.

Thamani halisi ya Mazao.
Wakati Heka moja wataalamu wanasema ina uwezo wa kutoa jumla ya Gunia 30 ambapo gunia moja kwa mujibu wa taarifa ya ya mwenendo wa bei za mazao ya chakula kutoka wizara ya kilimo kwa mwaka huu 2021 si chini ya Tsh 55000 ambapo kwa wastani wa gunia 30 mkulima atakuwa na shamba lenye ya thamani ya Tsh 1,650,000 hivyo ile tathimini ya juu ya Tsh 588,000 atakayolipwa kwenye hapo mkulima atakuwa amapata hasara ya Tsh 1,062,000 kwa hesabu ya 1,650,000-588,00=1,062,000.



Muhimu:-Hapa nimechanganua mfano wa mkulima wa kawaida anaetumia jembe la mkono sijaweka mkulima wa kisasa zaidi ambae anatumia Trekta,dawa za kuulia wadudu waharibifu na mbegu za kisasa ambazo huwa ghali hivyo gharama za uendeshaji hizo hapo ni kwa makadirio ya chini tu.


Idadi ya watu wanaotegemea Sekta ya Kilimo na Mifugo.

Matokeo ya muhimu ya sensa ya Kilimo mifugo na uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/2020 kama yalivyotolewa na mtakwimu mkuu wa serikali Dr Albina Chuwa yanaonesha kuwa kaya millioni 7.8 sawa na 65.3% ya kaya zote nchini zinajishughilisha na shughuli za kilimo.

Kati ya hizo kaya milioni 7.7 ni kutoka Tanzania bara na kaya 180219 ni kutoka Zanzibar,takribani 65% ya kaya hizo zinajihusisha na shughulisha na kilimo tu,33% wanajishughulisha na Kilimo na Mifugo na 2% wanajishughulisha na ufugaji tu.



Idadi ya Mifugo Tanzania.
Taarifa ya mifugo na Uvuvi ya mwaka 2019 ilionesha kwamba kuna idadi ya ng’ombe milioni 30.5, mbuzi milioni 18 na kondoo milioni 5.3 na kufanya idadi ya wanyama hao wanaoweza kuharibu mazao kufikia jumla ya milioni 53.8 hivyo ni sawa na kila Mtanzania amiliki wastani wa mfugo mmoja ukilinganisha na idadi ya watu milioni 44 kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.


Hitaji la Ardhi.

Hitaji la ardhi kwa matumizi mbalimbali nchini limekuwa likikuwa kila kukicha na hapa nitatolea mfano hitaji la ardhi kwa vijana kwa sababu ndio miongoni mwa kundi kubwa nchini ambapo ni sawa na 34.7 % kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi yam waka 2012.

Taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (nbs) ya taarifa kutoka utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi mwaka 2017/2018 kwa Tazania Bara pekee inaonesha 2% ya kundi la vijana wa miaka 15-35 wanahama kutoka mkoa hadi mkoa mwengine kwa mahitaji ya ardhi.


Suluhu.

Matumizi bora ya Ardhi.

Kwa mujibu wa wataalamu ni kwamba ng’ombe mmoja anatakiwa kuwa na eneo la heka 5 la kuchungwa kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo hali ilivyo kwa sasa inaonekana kwamba kuna idadi kubwa ya mifugo kuliko maeneo husika hali inayopelekea migogoro baina ya wafugaji na wakulima,n ahata ikitokea mkulima akilipwa baada ya mazao yake kuliwa na mifugo fidia hiyo haiendani na gharama zao za kuendesha kilimo pamoja na uhalisia wa thamani ya mazao kwa sasa.



Sheria ya mabadiliko ya thamani inasemaje?
Mwanasheria kutoka halmashauri ya wilaya ya Pangani Elibarik Msaky anasema,marekebisho ya sheria yanatokana na uhitaji wa jamii,muda na kubadilika kwa thamani ya shilingi,sasa kwenye hili wananchi wanaweza kutoa maoni yao kwa Mbunge ili awasilishe bungeni kama hoja binafsi kwa ajili ya serikali kuona umuhimu wa kubadilisha sheria hiyo”



Umuhimu wa Tafiti.
Wataalamu wanataja mbinu mbalimbali za kiteknolojia kwa ajili ya kuwafanya wafugaji waweze kufuga kwa tija,kwa maana ng’ombe kidogo kulingana na ukubwa wa eneo pamoja na kupata maziwa mengi pamoja na mifugo ambayo itakuwa na afya.

Miongoni mwa njia ambazo zinapendekezwa ni pamoja na kuhifadhi majani wakati wa mvua ili kuweza kuyatumia wakati wa kiangazi pamoja na upandaji wa majani,kituo cha cha utafiti wa mifugo Mkoani Tanga,TALIRI kimekuwa kikitoa elimu kwa wafugaji namna ya kufuga kisasa.



Hitimisho.
Ni wakati wa wafugaji kucha kufuga kimazoea na wafuate ufugaji wa kisasa,vijiji vitenge maenea ya ufugaji na kilimo kutokana na uhitaji na idadi ya mifugo iliyopo,sheria ya fidia ya mazao kwa mujibu wa waraka wa wizara ya Kilimo wa mwaka 2011 upitiwe na wabunge watoe mapendekezo ya mabadiliko ya sheria hiyo na pia wananchi waendelee kupaza sauti.





ROJAMIRO.

rajabumrope18@gmail.com

0626496734
 
Upvote 4
Ujinga wa sheria haibadiliki kila mwaka kuendana na thamani ya uchumi.
 
Data zako nyingi ni za uw0ng0





K
Just find that all data i mentioned to prove me wrong kabla hujaja na roho mbaya yako nishabeba tuzo nyingine za habari kama hujui

download.jpg
 
NAOMBA KURA YAKO NADHANI TUNAFAHAMU ADHA WANAYOKUTANA NAYO WAKULIMA PALE MIFUGO INAPOKULA MAZAO YAO FIDIA HUWA NDOGO SANA KULINGANA NA GHARAMA AMBAZO WAMETUMIA KUANDAA MASHAMBA AU KUWEKEZA KWENYE KILIMO
 
Back
Top Bottom