Shindano- Economic Empowerment for Tanzanians

Shindano- Economic Empowerment for Tanzanians

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
WAKUU NIMEONA HILI SHINDANO KWENYE BLOG MOJA HIVI, NIMEONA SI MBAYA NIKA-SHARE NANYI.




Taasisi isiyo ya kiserikali nchini Tanzania ya Economic Empowerment for Tanzanians (EET) ikishirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya nchini Ujerumani ya Glücklich Für Alle (GFA) inawaalika watanzania wote katika shindano la kuandika mchanganuo wa kibiashara (business plan) usiozidi kiasi cha shilingi milioni mia mbili(200) za kitanzania.

TUTAZINGATIA:

1. Uchanganuzi makini wa wazo la kibiashara
2. Utofauti wa wazo la kibiashara
3. Uhalisia wa wazo

SI LAZIMA:
1. Utumie lugha ya kiingereza pekee lugha zinazoruhusiwa ni pamoja na Kiswahili, Kijerumani na Kiingereza.
2. Uwe msomi wa Chuo Kikuu, kuanzia mshiriki wa Darasa la Saba na kuendelea anaruhusiwa

ZAWADI

(i) Mshindi wa kwanza, atapewa pesa taslimu za kuanzisha mradi wake, kiwango cha pesa kitategemea andiko lake.
(ii) Mshindi wa pili, atapewa kiasi cha fedha asilimia sabini na tano (75%) ya aliyoiandika kwenye mradi wake.
(iii) Mshindi wa tatu, atapewa asilimia hamsini (50%) ya aliyoiandika kwenye mradi wake.
Na (iv) Washindi wa nne, tano, sita, saba na wa nane watapewa kiasi cha fedha cha shilingi milioni 60 za kuanzisha mradi wao ambao utakuwa ni wa mshindi nambari nne.

KUMBUKA: Katika shindano hili pia kuna washiriki kutoka ujerumani, washiriki 25 wa kitanzania watapitishwa awamu ya kwanza na washiriki 25 watapitishwa awamu ya kwanza kutoka ujerumani ambapo kwa pamoja watawekwa kwenye academy moja kwa mwezi mmoja na kufundishwa mambo kadhaa hatimae watarudia tena kuandika mchanganuo wa kibishara kisha tutapata washindi nane (8) tu.

JINSI YA KUSHIRIKI
Email: tanzaniacompetition@gmail.com
Address:
maienweg 509, Hamburg-Germany

Imetolewa na,
Mwenyekiti wa EET,
Claus Paul.
 
Back
Top Bottom