Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta kwa wakazi wa Arusha Laota Elias akiserebuka mziki mara baada ya kuibuka mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta kwa mkoa wa Arusha wakati wa shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta wa jumla wa mkoa huo lililofanyika katika baa ya Bondeni iliyopo Kijenge juu jijini Arusha. Ushindi wa jumla wa Bw. Elias umekuja baada ya kuwabwaga washiriki wenzake watatu katika mtanange wa mwisho wa kuitambua ladha halisi ya bia hiyo na kuibuka Serengeti Masta wa mkoa wa Arusha. Shindano hilo la Serengeti Masta limezunguka katika baa mbalimbali jijini humo likiwaburudisha wateja wa bia hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa wateja.
Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta kwa wakazi wa Arusha Laota Elias akionyesha fedha taslim Tsh. 100,000/= alizopokea wakati wa shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta wa jumla wa mkoa huo lililofanyika katika baa ya Bondeni iliyopo Kijenge juu jijini Arusha. Ushindi wa jumla wa Bw. Elias umekuja baada ya kuwabwaga washiriki wenzake watatu katika mtanange wa mwisho wa kuitambua ladha halisi ya bia hiyo na kuibuka Serengeti Masta wa mkoa wa Arusha. Shindano hilo la Serengeti Masta limezunguka katika baa mbalimbali za jiji la Arusha likiwaburudisha wateja wa bia hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa wateja.
Mmoja wa washiriki wa shindano la kumtafuta Serengeti Masta wa jiji la Mbeya akitokea Power bar ya Mbalizi Maxmilian Majaliwa Kamanga akijaribu ladha tofauti za vinywaji vya kampuni ya SBL katika baa ya Mbeya Pazuri ambapo shindano la mwisho la kumtafuta mshindi wa jumla kwa mkoa huo lilifanyika mwishoni mwa wiki. Shindano hilo limezunguka katika baa mbalimbali jijini humo ambapo kwa ujumla shindano hilo limewafikia wahudumu zaidi ya 4000 Tanzania nzima katika kipindi cha miezi miwili ya kampeni na kuwafunza juu ya utoaji huduma kwa wateja.
Mshindi wa jumla wa shindano Serengeti Masta kwa jiji la Mbeya Faraji Mbwambo kutoka baa ya Gambino jijini Mbeya akionesha kitita cha fedha sh. 100,000 alizotunukiwa baada kuibuka mshindi wa jumla wa kuitambua ladha ya bia ya Serengeti Premium Lager kati ya vinywaji vitano vinavyozalishwa na kampuni ya SBL. Kampeni hiyo ya Serengeti Masta imewakutanisha wateja na mameneja wa bia hiyo katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia hiyo ambapo mameneja hao walitoa zawadi mbalimbali kwa washindi walioweza kuitambua ladha halisi ya bia hiyo katika kipindi cha kampeni.
Mshereheshaji na mratibu wa mashindano ya kumsaka Serengeti Masta jijini Mbeya Yassin Khalfan akizungumza na wateja waliohudhuria kushuhudia mpambano wa kumsaka mshindi wa jumla wa mkoa wa Mbeya katika baa ya Mbeya Pazuri mwishoni mwa wiki. Kampeni hiyo imefikia kikomo jijini humo baada ya kuzunguka katika baa mbalimbali katika kuwasaka washindi waliotambua ladha halisi ya bia ya Serengeti ambapo pia ilifanikiwa kuwafikia wahudumu zaidi ya mia tano katika baa tofauti tofauti waliopewa somo la utoaji huduma kwa wateja.