Shindano/Mashindano/Mchuano/Michuano

Nino

Member
Joined
Jun 21, 2007
Posts
38
Reaction score
1
Hamjambo.

Tafadhali mnisaidie kueleza kwa ndani zaidi tofauti za matumizi ya maneno yafuatayo:

Shindano/Mashindano - Mchuano/Michuano.


1) Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza (TUKI) inatafsiri:

"Mchuano: competition, match"

"Mashindano: 1 competition, contest" ("shindano" halimo)


2) Dictionary of Literary Swahili (Knappert) inatafsiri:

"Mchuano: match, game, contest, encounter"

"Mashindano: 1 contest, competition, race, match" ("shindano" halimo)


3) Comprehensive Swahili-English Dictionary (Mohamed A. Mohamed) inatafsiri:

"Mchuano: contest, match, competition"

"Mashindano: 1 competition, race, contest, match"

"Shindano: contest, competition"


4) Kamusi Kamili ya Kiswahili (Mdee, Shafi, Kiango, Njogu) inafasili:

"Mashindano: 1 mapambano katika mchezo baina ya timu zinazowania tuzo au kikombe fulani" ("shindano" halimo)

"Mchuano: mashindano baina ya timu au wachezaji katika michezo kama vile mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa mikono, riadha n.k."


5) Kamusi la Kiswahili Fasaha (BAKIZA) inafasili:

"Shindano: tendo la kupimana uwezo katika jambo k.v. mchezo; makabiliano yenye lengo la kuwania jambo baina ya pande mbili au zaidi" ("mashindano" halimo)

"Mchuano: 2 ushindani k.v. wa kimichezo kati ya timu au mtu na mtu; = mtuano"


Je, mnaweza kutoa mifano ya sentensi zinazotulazimisha tutumie neno fulani badala ya mengine?

Asanteni sana,
Nino
 
duu maana kiswahili huwa kinachanganya maneno sana hasa kwenye kutafuta maana zake karibu maneno yote huwa yanatumiwa sehemu moja tu..
 
Asante sana, ndetichia. Lugha zote huchanganya sana maneno mengi, yanayoitwa "visawe". Kwa hiyo "mchuano(mi)-shindano(ma)" ni visawe: "Michuano ya Olimpiki=Mashindano ya Olimpiki"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…