Shinikizo la damu (High Blood Pressure) inaweza sababisha kupoteza uono (vision). Kwa kifupi katika HBP mishipa ya damu mwilini hujibana (vasoconstriction) na hivyo kuhitaji moyo kufanya kazi ya ziada kuweza kusukuma damu kupita katika mishipa hiyo. Na hilo linaweza kupelekea mishipa hiyo kupasuka (kwenye ubongo kusababisha kiharusi au stroke) sehemu fulani fulani za mwili.
HBP inaweza kusababisha upotevu wa uono kwa njia zifuatazo:
- Kubana kwa mishipa ya damu ndani ya jicho (retina) hivyo kusababisha kukua kwa presha kwenye retinal blood vessels na hivyo kusababisha kupungua uono. Pia mishipa hiyo inaweza kupasuka pasuka (cumulative effect) na hivyo kupoteza uono taratibu mpaka kupofuka. Hili tatizo linaitwa Hypertensive Retinopathy.
- Kutokana na mabadiliko ya kimishipa ndani ya jicho, hii inaweza kusababisha optic nerve kuvimba na hivyo kushindwa kutuma message kwenye ubongo na kusababisha kutoona.
Matibabu/kinga kubwa ya Hypertensive retinopathy ni kucontrol tu HBP kwa njia mbali mbali ie. kutumia dawa, diet, na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kuhusu HBP. Pia kufanya check up ya macho mara kwa mara unapoenda clinic ya HBP kwa kutumia kifaa kinaitwa (Retinoscope). Daktari akikuangalia jicho kwa hiki kifaa anaona hayo mabadiliko na kukushauri jinsi ya kuyakabili.
NB: Tafadhali omba daktari akucheki kwa Retinoscope kila unapoenda kwenye clinic ya HBP au Kisukari. Ni haki yako.